Search This Blog

Monday, February 18, 2013

YANGA KUKUTANA KUJIPANGA NA MECHI DHIDI YA AZAM

JOPO la Kamati ya Utendaji,  Yanga linatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inashinda mchezo wake dhidi ya Azam FC kuwania taji la Ligi Kuu  Bara.

Yanga itakwaana na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili ijayo. Mchezo huo unatarajia kuwa mkali na wenye ushindani mkali kulingana na ubora wa timu hizo na pia nafasi kwenye msimamo wa ligi hiyo.
 

Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 33 nyuma ya pointi tatu na vinara Yanga. 

Katika mchezo wa kwanza, Yanga ilizaba Azam mabao 2-0. Mabao hayo yakifungwa na Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu.
 

Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu wa Yanga, Lawrance Mwalusako alisema kuwa mechi hiyo ni muhimu kwao kuhakikisha Yanga inashinda. 

"Baada ya mechi yetu na African Lyon ambayo tuliibuka na ushindi mnono, nguvu zetu zote tumezielekeza katika mechi ya Azam."
 

"Mchezo huo ni muhimu zaidi kwetu kushinda ili tuweze kuweka 'gap' la pointi tatu na Azam na kujiweka nafasi nzuri kutwaa ubingwa wa ligi." alisema Mwalusako.

2 comments: