Search This Blog

Wednesday, February 6, 2013

VIDEO HIGHLIGHTS: NIGERIA YAIPA KIPIGO CHA AIBU MALI NA KUTINGA FAINALI AFCON


Nigeria imetinga fainali baada ya kuicharaza Mali magoli 4-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Afrika.
Elderson Echiejile aliifungia magoli mawili ya kwanza katika dakika ya 25 na 30 ya mchezo.
Goli la tatu lilifungwa na Emenike katika dakika ya 44 baada ya mpira aliopiga kumgonga Momo Sissoko wa Mali.
Hadi mapumziko Nigeria ilikuwa ikiongoza kwa 3-0.
Ahmed Musa alizidi kuleta majonzi kwa mashabiki wa Mali alipofunga bao la nne katika 60.
Mali ilizidi kusaka bao, katika dakika ya 70 Cheikh Diarra aliifungia timu yake bao la kufutia machozi.
Nigeria kuingia nusu fainali waliwabwaga Ivory Coast 2-1, timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kucheza fainali kutokana na ubora wa wachezaji wake.
Nayo Mali iliwatoa wenyeji wa mashindano Afrika Kusini kwa njia ya mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu hizo kucheza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1-1.
Timu nyingine katika nusu fainali za Afcon ni Ghana itakayokwaruzana na Burkina Faso. Ghana waliitoa Cape Verde katika hatua ya robo fainali kwa magoli 2-0, huku Burkina Faso wakiifunga Togo kwa goli 1-0.
Sasa Nigeria inamsubiri mshindi kati ya Ghana na Burkina Faso zinazocheza mchezo wa pili wa nusu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika

3 comments:

  1. Nigeria wanaonekana wamejipanga this time kurudisha heshima yao,au ile ofa inachangia?

    ReplyDelete
  2. walijitambua wakaachana na wachezaji mabishoo na sasa wanarudisha heshima yao bravo nigeria hi ndo timu yangu ya ukweli africa ukiondoa ya taifa langu taifa stars niliumia kwa muda wa miaka kumi na tatu kila nilipo iona nigeria haifanyi vzr

    ReplyDelete
  3. I think this is the right time for Nigeria to be champions it has been a long time since they celebrated their AFCON victory.

    ReplyDelete