Search This Blog

Monday, February 11, 2013

SIMBA VS LIBOLO - TALIB HILAL ATUA ARUSHA KUONGEZA NGUVU

TIMU ya Simba inatarajia kurejea nchini Jumatano ijayo kutoka mjini Arusha ambako imeweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Libolo ya Angola.

Mechi hiyo imepangwa kufanyika Jumapili ijayo (Februari 17) kuanzia saa kumi na nusu jioni. Uongozi unafanya utaratibu wa kuiwezesha timu kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa walau mara moja kabla ya mechi hiyo ili kutoa nafasi kwa benchi la ufundi kutoa maelekezo mahususi kwa wachezaji kuhusiana na mechi hiyo.

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Talib Hilal, anaelekea Arusha leo ili kuongeza nguvu ya benchi la ufundi la Wekundu wa Msimbazi. Hii si mara ya kwanza kwa Talib kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi la Simba kwani alifanya hivyo pia miaka kumi iliyopita wakati klabu hiyo ilipocheza na Zamalek ya Misri na kufanikiwa kuitoa.

Talib Hilal hajaja kuchukua nafasi ya mtu yeyote kwenye benchi la ufundi. Amekuja kwa mapenzi yake kwa Simba na mara zote klabu inamkaribisha kwa vile uwezo wake kitaaluma, uzoefu wake na uwezo wake katika kuhamasisha unakubalika ndani ya klabu.

Simba SC inaomba washabiki na vyombo vya habari waisaidie klabu kwa kutotoa taarifa zenye kuashiria migogoro isiyokuwepo. Simba wanawakilisha heshima na hadhi ya Tanzania katika mashindano haya.

Unachoomba uongozi wa klabu ni uzalendo kwa taifa letu walau katika kipindi hiki ambapo kinachoangaliwa ni utaifa wetu. Uongozi unaomba wadau wake wa vyombo vya habari kuandika habari za kujenga umoja, mshikamano na uzalendo kwa Watanzania wote ili hatimaye Simba ifanye vizuri.

6 comments:

  1. Simba uozo mtupu ifike mahali unapoona umeshindwa uongozi toka,hizo ni kama mbio za vijiti.Julio anasema Ngasa kapigwa na msemaji anakanusha hapo Rage muongo nae hajaongea.

    ReplyDelete
  2. SIMBA INAREJEA NCHINI KUTOKA MJINI ARUSHA... KWANI ARUSHA IPO NCHI GANI???

    ReplyDelete
  3. Bila kuwatimua Rage Na Kaburu tutaendelea kukosa raha kila mechi,hawa wawili ndo tatizo simba.

    ReplyDelete
  4. Wanachama wa Simba na mashabiki ni vema tukaacha uchochezi na kuwa ki2 kimoja badala ya kutumia mda mwingi kujadili tofauti zetu chache tunatakiwa tuyakazanie yale mengi ambayo tunakubaliana kwa maslahi ya Simba , ikumbukwe kuwa uongozi huuhuu ndiyo ulioipa Simba ubingwa msimu uliopita.

    ReplyDelete
  5. well said hillary,hizi propaganda za chuki hazitatufikisha popote...kumbukeni hakuna aliye mkamilifu....tuungane pamoja kui-support Simba yetu...

    ReplyDelete
  6. oya simba inakuja nchin ikitoke Arusha? kuwen makin na kaz zenu

    ReplyDelete