Search This Blog

Monday, February 18, 2013

PAMOJA NA KUSHINDA 3-1, KOCHA WA AZAM HAJARIDHIKA NA KIWANGO CHA TIMU YAKE

LICHA ya Azam FC kuifunga timu ya Al Nasri ya Sudan Kusini mabao 3-1 juzi kuwania Kombe la Shirikisho, kocha Stewart Hall ameeleza kutoridhishwa na kiwango cha timu yake kiuchezaji.
Mwingereza huyo alisema mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kuwa timu hiyo imeshinda lakini ina kasoro nyingi za kiutendaji.
"Tumeshinda mechi nne mfululizo. Tatu zikiwa za ligi, lakini ukweli sijafurahishwa na jinsi timu inavyocheza."
Alisema kuwa bado kikosi chake kina matatizo makubwa ambayo amekuwa akijitahidi kuyarekebisha lakini bado yanajirudia mara kwa mara.
"Nashindwa kuelewa kwa nini tatizo hili linajiruadia mara kwa mara." alihoji kocha huyo.
Stewart alieleza kuwa tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi, timu hiyo imeshinda mechi zote lakini ukweli ni kwamba inashindwa kucheza dakika 90.
"Dakika 45 za kwanza timu inapoteza mwelekeo. Lakini baadae tunabadilika na nabadilika na kushinda. Mfano mzuri ni mchezo leo (juzi) na pia Mtibwa tulioshinda 4-1."
Aliongeza kuwa timu hiyo imekuwa akicheza vizuri dakika 45 za pili lakini za kwanza hupotea na kuruhusu wapinzani kufunga mabao kirahisi.
Katika mabao yote ambayo Azam imefungwa kwenye ushindi wake mechi nne zilizopita, imeruhusu mabao hayo manne dakika 45 za kwanza.

No comments:

Post a Comment