Search This Blog

Sunday, February 17, 2013

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 0 - 1 RECREATIVO


Full time Simba 0 - 1 Recreativo Libolo

Dk 90+5 Libolo wanacheza soka safi kwa kupiga pasi 25 ndani ya sekunde 50 bila Simba kugusa mpira.

Dk 90 Kinje anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu mbaya Henry Camara.

Dk 85 Simba inafanya mabadiliko, ametoka Boban ameingia Salum Kinje.

Dk 83 Libolo inafanya mabadiliko, ametoka Dario Cardoso ameingia Nuno Silva.

Dk 82 Boban anampiga kiwiko Pedro Ribeiro lakini mwamuzi hajaona. Ribeiro anatibiwa na kuendelea na mchezo. Simba 0-1 Libolo.

Dk 76 Antonio anaonyeshwa kadi ya njano kwa kuchelewa kutoka. Antonio alikuwa akikabidhi beji ya unahodha kwa Antonio Cassule.

Dk 76 Libolo inafanya mabadiliko, ametoka Antonio ameingia Henry Camara.

Dk 72 Libolo inafanya mabadiliko, ametoka Martins ameingia Andres Madrid.

Dk 67 Maieco Antonio anapiga shuti kali langoni kwa Simba lakini mpira unatoka nje kidogo ya goli.

Dk 76 Simba inafanya mabadiliko, ametoka Haruna Chanongo ameingia Ramadhan Singano 'Messi'.

Dk 62 Haruna Moshi Boban wa Simba anakosa bao la wazi akiwa jirani na lango la Libolo. Simba 0-1 Libolo

Dk 54 Dorivaldo Dias wa Libolo anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Mwinyi Kazimoto. Simba 0-1 Libolo.

Anatoka Mussa Mudde anaingia Amir Maftah

Dk 48 Simba inapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari la Libolo baada ya Almeida kumkwatua Ngassa.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Dk 45 HALF TIME! SIMBA 0-1 LIBOLO

Dk 41 beki wa Simba Komanbil Keita analala tackling lakini Maieco Antonio anauwahi mpira na kumpasia Martins anayepiga shuti kali linalodakwa na Juma Kaseja. Simba 0-1 Libolo

Dk 38 Bado mpira ni wa kushambuliana kwa zamu, Simba inaendelea kuimarika. Simba 1-0 Libolo

Dk 28 Libolo wamechangamka na kulishambulia kwa kasi lango la Simba japokuwa Simba wanaonekana kuleta uhai kidogo sehemu ya kiungo.

Dk 24 GOOO....! Joao Martins anaipatia Libolo bao la kwanza kwa kichwa akiunga krosi ya Carlos Almeida. Simba 0-1 Libolo

Dk 20 Pedro Ribeiro anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.

Dk 17 Simba wanazinduka na kutawala mchezo huku wakishambulia kwa kumtumia winga wake Mrisho Ngassa.

Dk 13 Libolo wanashambulia zaidi lango la Simba, wachezaji wa Simba wanaonekana bado wanausoma mchezo. Simba 0-0 Libolo

Dk 8 Dario Cardoso anapiga shuti langoni kwa Simba na mpira unagonga mwamba wa juu kisha mabeki wanaokoa.

Dk 2 Joao Martins anapiga shuti kali langoni kwa Simba lakini kipa Juma Kaseja anaudaka mpira.

Mpira umeanza hapa uwanja wa taifa.

FIRST ELEVEN- SIMBA SC... Kipa, Juma Kaseja... Mabeki, Shomari Kapombe, Nassor Chollo, Kommabil Keita, Juma Nyosso... Viungo, Mussa Mude, Haruna Chanongo, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba... Washambuliaji, Haruna Moshi, Mrisho Ngassa. MFUMO, 4-4-2... Simba v Recreativo, jioni uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Line up Libolo FC: Landu Mavanga, Carlos Almeida, Antonio Cassule, Pedro Ribeiro, Gamaliel Musumari, Manuel Lopes, Sidnei Mariano, Dorivaldo Dias, Joao Martins, Dario Cardoso, Maieco Antonio (C).

11 comments:

 1. poleni sana simba mmefungwa mbele ya ma nyuki angalieni atawakimbia kama alivyo wakambia africa lyon

  ReplyDelete
 2. kinje ni hold midfield anafaa kucheza ikiwa timu imeshinda goli zaidi ya tatu. kocha alichemsha kumchezesha kwa game hii.

  ReplyDelete
 3. UELEDI NA UKWELI WA MILOVAN + SIASA ZA CHUKI NA UONGOZI MBAYA WA SIMBA = TIMU MBOVU NA MATOKEO MABAYA..

  ReplyDelete
 4. Dhaira asipoangalia hapo kwa LEKADUTIGITE atasugua benchi mpaka msimu utaisha then akasimulie huko kwao kwamba kuna babu anaitwa KASEJA huyo anadaka mpaka friend match.

  ReplyDelete
 5. Simba inatuchefua.

  ReplyDelete
 6. timu pekee ya Tanzania inayoshiriki mashindano ya kimataifa

  ReplyDelete
 7. Ndg wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania. Naamini mtakubaliana nami kuwa kwa kweli Simba kuna matatizo kwa sasa! Si kawaida kwa Simba kufanya vibaya katika mechi za kimataifa hasa katika hatua za mwanzomwanzo! Soka la Tanzania hasa vilabuni linachanganywa na Siasa na uongo mwingi uliovuka mipaka ukijumulisha na ahadi hewa za mara kwa mara unapata jawabu kuwa bado tuna ugonjwa mkubwa katika soka la Tanzania. Viongozi pia kuingilia upangaji wa timu, kuwafukuzwa makocha huku wakishindwa kuwalipa stahili zao hadi waje kudai na mengineyo mengi ni viashiria vya kushindwa kufanya vizuri! Viongozi walioko madarakani wameshindwa kufanywa kinachohitajika kuiinua Klabu. Mfn ni aibu kwa klabu kubwa kama simba kukosa uwanja wake wa mazoezi na mechi. Tangu mwaka 1936 hadi leo ni miaka mingapi? Viongozi kadhaa wamekuwa wakikaririwa kuwa wana maono ya kujenga uwanja lkn hadi leo imekuwa ni ndoto za mchana! Swali ni kuwa kwa mwendo huu tutafika? Au tubinafsishe timu? naomba kuwasilisha! NURU SPORTS MSM

  ReplyDelete
 8. Rage, huu sio ujuzi wa mambo ya ghaibu, simba yako itafanya vibaya hadi ujirekebishe. Wazaramu walisema zilongwa mbali, zitendwa mbali. yaliandikwa haya toka vitabu vya ibrahimu na mussa.

  ReplyDelete
 9. Uongozi mbovu utafanya simba ishindwe katika kila mashindano. Mwenyekiti tambua kuwa penye ukweli uongo hujitenga. kuwa mkweli na fanya kazi na watu.fitina unazozikuza ndani ya simba hazitakupa mafanikio. Mwendo huu utakuja itia simba kwenye aibu kubwa. na huko ndiko simba inakoelekea.Yanga walipatwa na mambo makubwa hadi wakafikia kujipanga upya. angalia ndugu yetu Simba hiyo itakupasukia

  ReplyDelete
 10. Kocha aliechemsha alivyomtoa boban

  ReplyDelete
 11. Tunahitaji uongozi bora wa soka sio siasa rage na kaburu tunawashukuru pale mlipotufikisha tunaomba muwaachie watu wengne wenye mapenzi ya dhati na soka na walio na machungu na simba. By galashi

  ReplyDelete