Search This Blog

Tuesday, February 12, 2013

BRANDTS: AZAM WANATISHIA AMANI!

YANGA inashuka uwanjani Jumatano kuikabili African Lyon, lakini  Azam inampa presha kubwa kocha Ernest Brandts ambaye ameagiza wachezaji wake kuhakikisha wanaishushia mvua ya mabao Lyon  ili kuwadhibiti wana lamba lamba hao.
 Azam iliibamiza Mtibwa Sugar jana Jumapili mabao 4 – 1 na kukabana koo na Yanga kileleni. Timu zote hizo zina pointi  33, lakini Yanga inaongoza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakati Simba bado inachechemea  katika nafasi ya tatu baada ya kulazimishwa sare yabao 1 – 1 JKT Oljoro Jumamosi iliyopita jijini Arusha.
 Brandts amesema kuwa ligi sasa imefikia patamu  na hakuna kudharau timu hata moja ingawa kasi wanayokuja nayo Azam ni kubwa na inamuogopesha katika harakati zao za kutwaa ubingwa ingawa amedai kuwa  atawatuliza tu na Yanga itakuwa bingwa msimu huu.
Kocha huyo raia wa Uholanzi amewaambia wachezaji wake wajifunze kutokana na matokeo wanayopata Simba hivi sasa kwa kutambua kuwa  sasa ni muda wa kazi na  wanatakiwa kujituma zaidi ili kusaka amafanikiop.
 “Nafurahi  matokeo ya Simba kwa sabbau ni moja ya wapinzani wetu wakubwa ingawa Azam nao wanakuja spidi hivyo  lazima tujihadhari maana wameamsha mapambano makali ambayo hatuna budi kuyashinda.
 “Matokeo ya Simba kuna kitu yanatufunza , Lazima wachezaji wanatakiwa wajitume na kuiacha mbali ikiwa kushinda kila mechi. Hakuna mechi rahisi kwani hivi sasa kila timu inakomaa haitaki  kufungwa ingawa mikakati yetu ni kuhakikisha tunashinda  na kutangaza ubingwa mapema” alisema Brandts.
 Aliongeza” Tunacheza na African Lyon Jumatano( kesho) hatuwezi kuwadharau licha ya wao  kupoteza michezo yao yote ya raundi hii lakini  hii ni soka wanaweza wakaja wakabadilika na ukizingatia kuna wachezaji  wane walitoka kwetu hivyo haitakuwa mechi rahisi.
 “ Lakini nasisitiza kwa wachezaji wangu hasa washambuliaji kuhakikisha tunashinda mchezo huo tena kwa mabao mengi ili  kupambana na Azam kileleni” alisema  Brandts.
 Vita ya ubingwa  imeonekana kupamaba moto katika timu tatu Yanga, Azam na Simba ingawa wekundu hao wa Msimbazi wameonekana kuchechemea katika mbio hizo.
 Ingawa Yanga inaonekana ina  ahueni zaidi katika michezo yake 11 iliyobaki kwani mechi  sita ndio zinaonekana zitaipa shida timu hiyo katika harakati zake za kuwania ubingwa wakati Azam ina mechi  saba ngumu pia wakati Simba ndio ina kazi kubwa zaidi kwani ina mechi  tisa ngumu.
 Yanga ina mechi ngumu dhidi ya  JKT Ruvu, Azam, Kagera Sugar, JKT Oljoro, Coastal Union na Simba ingawa  inapata haueni kwani mechi nyingi inacheza kwenye Uwanja wa nyumbani wakati Azam ina kazi dhidi ya  JKT Ruvu, Yanga,  Ruvu Shooting, Simba, Coastal na Oljoro na Mgambo Shooting.
 Simba yenyewe itabidi ifanye kazi ya ziada  kuziadabisha  Prisons, Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Kagera, Azam, Toto, Mgambo Shooting  na Yanga kama kweli inataka kutetea  Ubingwa wake

No comments:

Post a Comment