Sekretarieti
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepokea barua ya
Serikali ikielezea uamuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara kutengua uamuzi wa Msajili wa Klabu na
Vyama vya Michezo nchini kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo
la 2012.
Baada
ya kupokea barua hiyo jana alasiri (Februari 25 mwaka huu),
Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza
kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kujadili tamko hilo.
Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya TFF kitafanyika Jumamosi (Machi 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mambo muhimu katika kuboresha soka la Tanzania:
ReplyDelete========================================
• Idadi ya timu katika ligi kuu soka Tanzania bara ziongezeke hadi 25 ili kukidhi uwiano wa idadi ya watanzania.
• Kila taasisi imiliki timu moja tu katika ligi kuu ili kujenga soka ya ushindani wenye tija.
• Uwekezaji na promosheni uongezeke katika ligi la daraja la kwanza ili kujenga ushindani na kuibua vipaji
• Vilabu vyote viwekeze katika rasimali na menejimenti mahiri na makini katika tasnia ya soka.
• Kuwekeza katika ubunifu wa ligi ya timu za asasi za ulinzi na usalama.
• Kuwekeza na kuhifadhi rekodi za washiriki wa mashindano ya asasi za elimu kuanzia ngazi ya shule za msingi.
• Manispaa na asasi zote za michezo ziwekeze katika viwanja vya michezo ikiwa ni sehemu muhimu katika huduma za kijamii