Search This Blog

Thursday, January 31, 2013

CANNAVARO - VIWANJA VIBOVU VYA BONGO VINANIPA TAABU SANA


BAADA ya kutamba na viwanja vya kisasa vyenye ubora wa 'kapeti' vya Uturuki, beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema mabadiliko ya viwanja vinampa wakati mgumu, ingawa  anajitahidi kuzoea mazingira ya viwanja chakavu vya Bongo.

Nahodha huyo msaidizi wa Yanga, aliliambia tovuti hii jijini Dar es Salaam kuwa bado anafikiri ni tatizo ambalo linaweza kuwa sababu ya matokeo mabaya ya timu hiyo hasa kwa mechi za mikoani. 

"Kweli inatuweka kwenye wakati mgumu. Leo unacheza uwanja mzuri wa Taifa ambao una ubora, ghafla tena unacheza uwanja chakavu wa Sokoine mjini Mbeya. Ni tatizo," alisema Cannavaro.

Alisema anafikiri ni sahihi kwa timu hiyo kufanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam ili kuyazoea mazingira ya viwanja chakavu vya mikoani.

"Nafikiri tumetoka Uturuki kambi ya wiki mbili tulifanya mazoezi kwenye viwanja vyenye ubora sana. Lakini tumerudi kwenye viwanja chakavu lazima tuzoee ndio maisha yetu haya."

Hata hivyo, Kocha wa Yanga, Ernie Brandts alisema bado hajafurahishwa na Uwanja wa Bora na kuutaka uongozi wa timu hiyo kutafuta uwanja mwingine wa mazoezi wenye majani ili kuepusha wachezaji wake kuumia na hasa wakati Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili ukiwa tayari umeanza kushika kasi yake.

2 comments:

  1. soka la bongo upuuzi mtupu,just imagine gharama za safari ya uturuki,kuanzi maandalizi,tiketi,viza,malazi,na mengineyo watu karibia 30,chukuria kila mtu katumia dola elf 7 cku zote hizo 14 uturuki jumla ni dola 210000,hizo pesa ukizileta kwenye madafu ni kama mil 350 ambazo wengeweza tengeneza au wengeweza weka kapeti uwanja wa kaunda na kuwa na kiwanja bora cha mazoezi kama chamazi,tuombe mungu alichosema mwenyekit kuhusu uwanja kitimie,njoo msimbaz sasa chukua kiasi hicho hicho walichotumia yanga the same story to simba,ila huku msimbaz plus na mauzo ya okwi wanashindwaje kuwa na kiwanja bora cha mazoezi chenye hazi yao?this is africa in tanzania bora mambo yaende kilichobaki wachezaji wetu wasilalamikie viwanja cos walitokea kwenye viwanja hivyo hivyo vibozu wanachotakiwa ni kupambana na kwenda cheza mpira nje ya nchi kwenye viwanja na vitendea kazi vilivyo bora.

    ReplyDelete