Search This Blog

Friday, January 18, 2013

BLACK LEOPARDS YATUA TAYARI KUIPIMA YANGA KESHO TAIFA


 
 Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili mchana wa leo kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius kambarage Nyerere.
Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waratibu wa shindano hilo,kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Pichani kushoto ni Shaffih Dauda,Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga,Mtangazaji wa kipindi cha Sports Extra,Mbwiga Mbwiguke,Mdau Juma pamoja na Stuart
 Nahodha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili na kikosi chake kizima leo mchana tayari kwa kupambana na timu ya Yanga Sports Club,kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Waratibu kutoka Prime Time Promotions Ltd,Shaffih Dauda pamoja na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo Godfrey Kusaga wakifanya mawasiliano leo mchana mara timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini ilipowasili kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
 Shaffih Dauda akiwa ameambatana kocha wa timu ya  Black Leopards ya Afrika Kusini,Abel Makhubele mara baada ya kuwasili leo mchana kwenye uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere.
 Wachezaji wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiingia kwenye basi kubwa la timu ya Yanga,wayatarajia kumenyana nayo hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa,Jijini dar.
 Kikosi cha  Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwasili mapema leo mchana kwa ndege ya shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. kambarage Nyerere.Picha zote na JIACHIE BLOG.
======  ======= ======= =======
WAKATI mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga kesho watacheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, kocha wa Black Leopards ametema cheche na kusema wataibuka na ushindi mkubwa kutokana na uzoefu wao wa mashindano ya Kimataifa.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni na maandalizi yake yamekwisha kamilika huku waandaaji wakipunguza viingilio ili kuwawezesha mashabiki wengi kufika.
Mratibu wa mechi hiyo, Shafii Dauda wa Prime Time promotion alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na wamepunguza kiingilio cha shs 5,000 na shs 7,000 na kuwa cha shs 3,500 ili kuwafanya mashabiki wengi kuona mechi hiyo.
Viingilio vingine ni shs 7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa, wakati VIP C ni shs 15,000 , VIP B shs 20,000 na VIP A shs 30,000
Dauda alisema kuwa Black Leopards wamewasili na kutamba kushinda mechi hiyo kutokana na uzoefu waliopata katika mashindano mbali mbali ikiwa pamoja na kombe la Shirikisho.
Kocha wa timu hiyo, Abel Makhubela alisema kuwa wanauzoefu wa siku nyingi na walifanya ziara nchi mbali mbali katika afrika na kuja Tanzania ni moja ya faraja kwao.
“Ziara hii ziara yetu ya kwanza Tanzania, tumefanya ziara nchini Zimbabwe na nchi nyingie, tulipata matokeo mazuri na vile vile tunatarajia kupata matokeo mazuri hapa, nimekuja na wachezaji wangu wote wa kikosa cha kwanza, jumla ya wachezaji ni 23, mashabiki watarajie mchezo mzuri,” alisema Makhubela.
 Alisema kuwa wanaijua Yanga na Simba ni moja ya timu nzuri na maarufu bara la Afrika na hivyo wamejiandaa kwani ni kipimo kizuri cha ligi ya kwao ambayo ipo katikati..

1 comment:

  1. Great clouds kwa kutuletea timu toka Africa Kusini...achaneni na huyo jamaa wa bongostaz anapaka kwenye blog yake kuwa hiyo timu siyo chochote...na inaangaika kushuka daraja, ni bora Yanga wangecheza na Costal...huyo jamaa mpira sijui anaujulia wapi...kusafiri kwenye katoka na Azam Congo na Uganda basi anajiona mjanja sana. Big five clouds media.
    Mdau
    South Africa

    ReplyDelete