Lionel Andres Messi anazidi kuishangaza dunia kwa uwezo wake mkubwa karika soka. Lionel Messi aliezaliwa miaka 25 huko Rosario , Argentina. Messi ni mtoto wa Mzee Jorge Horacio Messi ambae alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha Chuma na mama yake Celia Maria Cuccitti. Kwa upande wa Baba yake Messi anaasili ya Italy tokea mji mmoja unaitwa Ancoma, ambako ilikuwa ni asili ya babu yake aitwae Angelo Messi aliehamia Argentina mwaka 1883. Messi ana kaka wawili na dada mmoja.
Katika umri wa miaka mitano Leo Messi alianza kucheza soka katika club ya Grandoli. Hii ilikuwa klabu ya mtaani kwao iliyokuwa inasimamiwa na Baba ake. Mwaka 1995 Messi alihamia katika klabu ya Newell's Old Boys iliyopo katika mji wake wa Rosario.
Messi akiwa na miaka 11 |
Raxach alikubali kumpa Messi mkataba na Barcelona, akiwa hana karatasi yoyote mkononi alimwandikia mkataba wa kwanza Messi katika Leso.
Hatimaye Barcelona walikubali gharama za matibabu ya Messi kwa masharti kuwa ahamie Hispania. Bila kipingamizi Messi na Baba yake wote wakahamia Hispania na Lionel akaanza kuitumikia klabu ya Barcelona akiwa katika katika shule ya vipaji ya klabu hiyo iliyo maarufu sana kama La Masia.
Messi na Macarena |
Inasemekana Messi amewahi kuwa na uhusiano na mwanadada Macarena ambae naye anatokea katika mji wa Rosario. Messi alitambulishwa kwa Rosario na baba yake Rosario kipindi aliporudi kuuguza majeraha yake kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia 2006. Messi pia alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamitindo wa Argentina mwanadada Luciana Salazaar.
Januari 2009 katika mahojiano ya kipindi "Hat-Trick Barca'" cha Canal 33 Messi alisema anauhusiano na mwanamke mmoja hivi (hakumtaja jina) na anafuraha kuwa nae swali hilo lilikuja baada ya Messi kuonekana katika sehemu mbalimbali na mwanadada Antonella Roccuzzo. Juni mwaka 2012 Messi akicheza mechi dhidi ya Ecuador alifanikiwa kufunga goli, alishangilia Goli hilo kwakuweka mpira ndani ya jezi yake kuashiria kuwa mpenzi wake ni mjamzito. Siku kadhaa baadae ikaripotiwa na vyombo vya habari kuwa mpenzi wake ana ujauzito wa wiki 12 (miezi 3). Mnamo Tarehe 2 Novemba mwaka 2012 mtoto wa kwanza wa Messi alizaliwa na kupewa jina la Thiago.
Messi akishangilia bao dhidi ya Ecuador |
Messi ana ndugu wawili ambao waacheza mpira. Maxi anaichezea klabu ya Club Olimpia nchini Paraguay na Emmanuel Biancucchi. Pamoja na kuishi Spain kwa muda mrefu ila Messi hajaacha kupakumbuka Rosario. KIla mara hutembelea mji huu na pia ana mawasiliano na marafiki na ndugu kadhaa wanaoishi katika mji huo. Inasemekana wakati mmoja Argentina ilipokuwa ikifanya mazoezi mjini Buenos Aires. Messi aliendesha mwendo wa masaa matatu baada ya mazoezi kwenda Rosario kula chakula cha jioni na kulala na kesho yake kugeuza mapema kabla ya mazoezi. Messi bado anamiliki nyumba yao ya zamani ambako alikuwa anaishi na familia yake japokuwa hakuna mwanafamilia anayeishi hapo siku hizi.
Mwaka 2007, Messi ameanzisha Charity Foundation kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji.
Messi alitangazwa kuwa balozi wakujitolea wa UNICEF katika maswala ya kupigania haki za watoto. Barcelona nao wako nyuma wanamsaidia messi katika hili kwakuwa Barcelona na Messi wana uhusiano mzuri.
Messi alianza kuichezea timu ya wakubwa ya Barcelona tarehe 16 Novemba mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 145 katika mchezo wa kirafiki kati ya Barcelona na F.C Porto ya Ureno.
Miezi michache baadae Frank Rijkaard kocha wa barcelona kipindi hicho alimpatia Messi nafasi ya kucheza ligi ya Spain dhidi ya RCD Espanyol akiwa na Umri wa miaka 17 na siku 114 hivo kumfanya Messi kuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kuichezea Barcelona na mdogo kabisa kuichezea Barcelona katika ligi. Rekodi ambayo baadae ilikuja kuvunjwa na Bojan Krikic. Goli la kwanza la Messi katika timu ya wakubwa alilifunga dhidi ya Albacete Balompie mwezi Mei mwaka 2005. September mwaka huohuo Messi alipata urai wa Spain.
Baada ya hapo amekuwa akicheza kwa mafanikio makubwa. Messi katika kipindi hichi chote toka alipoanza kuichezea Barcelona amepata mafanikio mengi. Mafanikio Binafsi kama mchezaji na Mafanikio ya timu pia.
Messi ameweza kuvunja rekodi nyingi ambazo ziliwekwa na magwiji wa soka wa zamani. Tukianzia katika klabu yake Messi ameweka rekodi ya kuwa mchezaji anaeongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo akiwa na magoli 283 na pia ni mchezaji alieifungia Barcelona mabao mengi katika ligi ya Hispania uku akiwa na mabao 192. Messi anashikilia rekodi ya klabu yakufunga Mabao mengi kwenye msimu mmoja akiwa amefunga magoli 73 katika msimu wa 2011-2012. Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika mashindano ya ulaya akiwa na magoli 57 na 56 katika ligi ya mabingwa ulaya. Messi anaongoza listi ya mchezaji aliefunga magoli mengi katika Spanish Super Cup akiwa na magoli 10.
Messi ana rekodi ya kuwa mchezaji alieifunga magoli mengi kwa msimu mmoja katika michuano ya mabingwa ulaya akiwa na magoli 14, Messi huyuhuyu ana rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya akiwa amefunga 5 katika mechi dhidi ya Bayern Leverkusen msimu wa 2011-2012. Messi ana rekodi pia yakufunga hat-tricks nyingi ndani ya msimu mmoja akiwa amefunga hat-trick mara 8 msimu wa 2011-2012. Na bila kusahau Messi anashikilia rekodi ya Barcelona ya kufunga magoli mengi katika ile michuano ya klabu bingwa ya dunia akiwa na magoli 4.
Kwa ujumla Messi anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya hispania akiwa amefunga magoli 50 katika msimu mmoja. anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya mabingwa huko akiwa a magoli 14 na pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliefunga magoli mengi ndani ya msimu mmoja akiwa na magoli 73 katika mashindano yote. Messi hajaishia hapo, Jana tarehe 09-Dec-2012 Messi amevinja rekodi ya mkongwe Gerd Muller ya mabao 85 katika mwaka mmoja ambayo ilidumu kwa miaka 40. Messi amefunga goli la 85 na 86 jana akiisaidia Barcelona kushinda mchezo wake dhidi Real Betis. Messi ameweka rekodi hiyo mpya uku akiwa na michezo mitatu mpaka mwisho wa mwaka.
Messi bado ana rekodi zake binafsi. Messi ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka 3 mfululizo (209,2010,2011) na mwaka huu yuko katika ile tatu bora. Messi anashikilia tuzo ya mfungaji bora wa bara la Ulaya ya mwaka 2010 na mwaka 2012. Mshambuliaji bora wa ligi ya Hispania mwaka 2009,2010,2011,2012. Mchezaji bora wa ligi ya hispania mwaka 209,2010,2011,2012. Mfungaji bora ligi ya Mabingwa ulaya mwaka 2009,2010,2011 na 2012. Man of the match fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2011.
SOURCE:http://valetyno.blogspot.ca/
huyu sio mtu wa kawaida ! of coz hakuna wa kumlinganisha nae by the way anastahili kuja chelsea !
ReplyDeleteMessi has no Mercy!!
ReplyDeletehuyu kijana anatisha ila mafanikio yake mengi huchandiwa na nguli wa la masia soccer academy yaani XAVI na INESTA
ReplyDeleteKaka Shaffih asante sana kwa hili.
ReplyDelete