Search This Blog

Monday, December 3, 2012

KALI YA WIKI - KAMA ALIVYOAHIDI: MOURINHO AINGIA UWANJANI DAKIKA 40 KABLA YA MECHI ILI WAZOMEAJI TIMU WAMZOMEE MPAKA WATAKAPOCHOKA

 

Wakati wa mkutano wake wa waandishi wa habari Ijumaa iliyopita, Jose Mourinho alitoa ujumbe kwa mashabiki wa Real Madrid ambao walikuwa na hasira dhidi ya timu kushindwa kukimbizana na kasi ya Barcelona msimu huu. Alisema angeenda uwanjani mapema dakika 40 kabla ya mechi dhidi ya Atletico Madrid na wale mashabiki "wenye hasira na hupenda kuzomea watapata nafasi ya kunizomea vyovyote watakavyo."

Jumamosi ikafika, muda ule ule dakika 40 kabla ya mechi kuanza, Mourinho alitoka ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo, akawapita wapiga picha na akasogea mpaka ndani ya uwanja kuwapa nafasi mashabiki ambao tayari walishaanza kuingia uwanjani kumzomea kama ambavyo wanapenda kufanya wakati wa mechi.
Baadhi ya washabiki walimshangilia, wengine walimzomea huku wengine wakilitaja jina lake na kumsifu.

Hii hapa ndio video

3 comments:

  1. Mbona haiplay kaka....iweke tena

    ReplyDelete
  2. Kaka uwe una preview habari zako,,sasa video haichezi

    ReplyDelete