Songombingo la kupotea kwa mchezaji Mrisho Ngassa bila taarifa yoyote kwa vilabu vyake vya Simba na Azam FC, na klabu inayomtaka kumsajili ya El Merreikh ya Sudan limechukua sura mpya jioni hii baada ya msemaji wa klabu ya El Merreikh kuzungumza na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.
Akizungumza na Shaffih Dauda, shekhe Idrissa amesema kwamba El Merreikh imeshakubalina kimsingi na vilabu vya Azam FC na Simba SC na mchezaji na kilichokuwa kimebakiwa na kutia saini kwa mikataba pamoja na kufanya vipimo vya afya ili mchezaji huyo aweze kujiunga na timu hiyo tajiri ya Sudan, lakini muda mfupi baada ya kufika Dar es Salaam mchezaji huyo amekuwa mafichoni - akiwa hapokei simu na muda mwingine anazima bila kutoa taarifa zozote kwa vilabu husika.
"Mrisho Ngassa tulikuwa tumeshafanya nae mazungumzo vizuri na tukakubaliana na ikabakia kumalizana na vilabu vya Simba na Azam, lakini sasa tukiwa tayari tumemalizana na vilabu mchezaji mwenye amekuwa akifanya vitendo visivyo vya kistaarabu, simu yangu hapokei na muda mwingine anaaizima kabisa. Hili sio jambo zuri kabisa kwake na kwa mpira wa Tanzania kiujumla. Anaharibu sifa ya wachezaji wenzie wa kitanzania, ni vizuri angepokea simu na kutueleza kama dili linawezekana au tofauti, kuliko kutuacha sisi tukipoteza muda kuwepo hapa Tanzania. Kwa tabia hii ya Ngassa tumefikia maamuzi ya kwamba mpaka kesho asubuhi kama mchezaji atakuwa hajapatikana then tutasitisha uhamisho wa mchezaji huyu na kuangalia sehemu nyingine mbali na Tanzania." - Alimaliza Shekhe Idrissa.
Taarifa zilizoenea ni kwamba Ngassa hataki kwenda El Merreikh baada ya kushawishia na viongozi wa Kulwa ili aendelee kuwepo Simba mpaka mkopo wake utakapoisha mwakani na aweze kujiunga na klabu hiyo yake ya zamani.
Ni watu wachache sana wanao watakia mema wenzao,ngassa hana washauri wazuri,kwa manufaa ya carrier yake hata km kuna timu itampa dau sawa,na elmerekh,bado angetakiwa kwenda kule,,kuna vitu vingi sana angejifunza,lakini tusimlaumu sn inawezekana anaangalia pesa zaidi kuliko carrier yke kwa ujumla.Lakini afahamu ndio anazidi kuwachimbia kaburi wanaomfata..
ReplyDeleteChezea kupima afya wewe?
DeleteHuku bongo kwenda angaza tabu,itakuwa kupimia sudani?
Wengi wao ni wagonjwa na ndio maana wataendelea kuwa wahapahapa.
Wewe umepima? Tusinyosheane vidole, sisi wote ni marehemu watarajiwa....L
Deletekaka mi nilipokuwa natoa la moyoi kuwa hawa watu wanahitaji viboko nilikuwa namaanisha kiukweli na kiuasilia zaidi, maana hebu ona katoto kajuzi leo kanajiona keki kwa sababu ya kulaghaiwa na watu wachache sana wasio na mapenzi na timu yangu ya taifa sasa hebusema na wewe ni mchezo gani huu wa kipuuzu ambao hawa wasiojua mchezo wanataka kuufanya?m au hii tabia ambayo imekuwa ikifanyika hapa kwetu wanataka kuipeleka na kwenye nchi nyingine? mi nasema TUUNGANE KWAPAMOJA TUKEMEEE HUU MCHEZO, MARA YANGA, AZAM AU SIMBA JAMANI HUU MCHEZO UNAUA VIPAJI VYA VIJANA WETU NA HASA UKIKUTA KIJANA NAE HANA WASHAURI WA MAANA NDIO KABISAAAAAAAAAAAAA, INANIUMA SANA JINSI CARRIER HII INAVYOCHEZEWA NA WAJINGA WACHACHE
ReplyDeleteHizi fitna za simba na yanga zinapotosha sana wachezaji, na tatizo kubwa viongozi wetu wa vilabu wamekaa kushibisha matumbo yao tu matokeo yake ndo haya sasa
ReplyDeleteHuyu Mrisho Ngassa ni bogasi kabisa, huo umalaya wa uswahilini ndio unaomsumbua, pumbafu kabisa
ReplyDeletewewe nani anakuamlia maisha yako? why does it hurt you, who decides your destine? you just believe kwamba Ngasa ana akili timamu ya kumwezesha kuishi maisha atakayo. katika maisha wakati mwingine pesa si kila kitu, you can have all the world but still ukawa unhappy, mwacheni ajiamlie maisha yake, after all akiyapatia au akayashindwa maisha ni yeye, you won't be there to help. so heshimu mawazo yake an uamuzi wake
DeleteNafikiri Samatta ni wa pekee maana kwa umri wake kukubali kwenda timu kubwa ugenini nafikiri hata kichwani yuko vizuri anawazia kuperform kwanza ndio maana amepiga hatua wengine wapowapo tu.
ReplyDeleteTusimlaumu Ngasa kujua kilichotokea. Mpaka muda huu tumesikia taarifa za upande mmoja tu. Inawezekana hili dili lilikuwa siri, maana hata simba (pamoja na kwamba Ngasa yupo huko kwa mkopo) hawakupewa taarifa ya kuuzwa kwa Ngasa. Kuna usalama hapo??
ReplyDeleteHuyu Ngassa ni mshenzi kabisa huwezi kupata bahati kama hiyo alafu unaichezea na hao Yanga ni watu wasiowatakia mafanikio wachezaji mara nyigi wanataka kuona wako kwenye timu yao isiyo na mafanikio yoyote zaidi ya kuishia kwenye kombe la Afrika Mashariki kwa mizengwe tu. Kila mchezaji wao anapotakiwa na timu za nje wanamkatalia kwa kuogopa goli tano. Hizo zinabaki kwenye historia hazitafutika kama ambavyo goli sita wameshindwa kuzifuta.
ReplyDeleteWandugu tatizo kwa wachezaji we2 ni upeo mdogo Wa kufikiri(kukimbia shule)
ReplyDeletekuna kila ulazima kwa TFF kuwasaidia wachezaji kama akina Ngassa, wasirubuniwe na vikundi au vilabu visivyo na taswira ya maendeleo kwa wa wachezaji kama hawa!
ReplyDeleteSAKATA LA NGASA, EL MERREIKH, AZAM NA SIMBA
ReplyDeleteTukumbuke mambo 7 muhimu:
1. Ngasa kabakiza miezi 5 kumaliza mkataba wake awe huru na baada ya hapo timu ikimtaka anaweza kuchukua pesa zote mwenyewe.
2. Azam iliamua kumuuza bila yeye na Simba kujua - ushahidi ni kauli ya Zacharia Hans Pope kuwa "eti walijitahidi kumsemea Ngasa na El Merreikh wakaongeza signing fee kutoka dola 30,000 hadi dola 75,000"
3. Simba ilimchukua kwa mkopo wa lazima toka Azam na wala si mali yao kumwamria kwa kwenda na kudai "share" ambayo Ngasa hapati kama shukrani ya kuwafanyia biashara. Tukumbuke vilabu vinayouza pia huwapa wachezaji sehemu ya mapato ya kuwauza.
4. Azam ilimrushia vyake na kusema aende kwa mkopo au akae becnhi hadi mkataba wake uishe (tena alihukumiwa bila mashauri yoyote baada ya yeye kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga)
5. Yanga, Simba, Azam nk nao ni muhimu kujiimarisha kwa kuwa na wachezaji bora ili kuhimili vishindo vya mechi za kimataifa na kufikia viwango vya TP Mazembe, Al-Ahly, Kaizaer Chiefs, Esperence, etc.
6. Tresor Mputu wa TP Mazembe alikataa mara kadhaa kujiunga na Arsenal na Glasgow Celtic na kuamua kubaki Mazembe ili kuifanya Mazembe klabu kubwa Afrika kulingana na vision ya klabu na mmiliki Moise Katumbi.
7. Vilabu vyetu vijifunze kuwa na ambition ya kuwa bora zaidi Afrika na dunia hivyo kuwa na mikakati sahihi ya kujijenga ikiwa ni pamoja na kubakiza mastaa wako (akina Kapombe, Niyonzima, nk) na kuwaleta wengine ili kutogeuka ni Academies tu kama ambavyo Arsenal wanahangaika sasa.
Nawasilisha!!!