Search This Blog

Monday, December 10, 2012

BREAKING NEWS: HATIMAYE SIMBA NA AZAM WAFIKIA MAKUBALIANO YA KUGAWANA FEDHA ZA USAJILI ZA NGASSA

Baada msuguano wa takribani wiki mbili kuhusu nani hasa anastahili hasa kuchukua fedha za usajili wa mchezaji Mrisho Ngassa kati ya vilabu vya Simba na Azam, hatimaye leo hii umepatikana muafaka.

Viongozi wa pande mbili za vilabu hivyo wamekutana na kukubaliana kwamba watamuuza mchezaji Mrisho Ngassa kwenda klabu ya El Merreikh kwa ada ya usajili ya $100,000 na fedha hizo zitagawanywa kwa Simba na Azam FC.

Kwa upande wa mchezaji mwenye Mrisho Ngassa atapokea kiasi cha $75,000 kama gharama ya usajili kwa mkataba wa miaka miwili, na pia atalipwa kiasi cha $4000 kama mshahara kwa kila mwezi.

Simba na Azam zilikuwa zikigombana kuhusu nani hasa alikuwa mmiliki halali wa mchezaji huyu.

8 comments:

  1. Simba njaa imewazid,mchezaji sio wenu mnadai fedha!uzeni wachezaji wenu magalasa!
    #samahani lakini

    ReplyDelete
  2. khaleed azam walimuona ngasa galasa,karudisha kiwango simba,simba ndo njia panda ya mafanikio ya wachezaji hata wenyewe wanajua,ukitaka kusonga mbele nenda simba hakuna kubaniana.

    ReplyDelete
  3. Pongezi kwa Simba na Azam kwa makubaliano,kwa ajili ya manufaa ya Ngassa na Taifa.

    ReplyDelete
  4. Kwa mfano, Mchezaji yupi galasa unayemwona Simba...?

    ReplyDelete
  5. Simba wamezoea kufanya mikataba ya kihuni,mambo yanapokuwa mabaya wanaanza kutapatapa,poleni sana!

    ReplyDelete
  6. Kutangaza maslahi ya mtu kama ilivyofanyika kwa Ngasa sio sahihi. Hata viongozi wetu wa serikali ambao wanalipwa kwa fedha za walipa kodi hatutangaziwi mishahara yao. Hata mwandishi wa habari hizi nadhani hatakubali kuanika maslahi yake namna hii. Ninaamini mwandishi anafahamu vyema sababu za kutotangaza mishahara kwa hiyo hakumtendea haki Ngasa!!!

    ReplyDelete
  7. wacha cmba wachukue hak yao. kwani walimpa gari . na mishahara pia .

    ReplyDelete