Search This Blog

Tuesday, November 13, 2012

SALVADOR CABANAS - MWANASOKA ANAYEISHI NA RISASI KICHWANI

Mwezi January 2010, Salvador Cabanas aliinuka kutoka kwenye siti yake ndani ya Bar na kwenda chooni. Mwanaume mmoja akaungana nae kwenda maliwatoni kujisaidia na wakiwa wapo ndani ya vibanza vya kujisadia haja ndogo yule mwanaume akamwambia Cabanas: "Nakupiga risasi." Cabanas akamjibu: "Kama unaweza nipige hiyo risasi."
Ukasikika mlio mkubwa 'BANG!!!

 
Miaka miwili sasa imepita amerudi kucheza soka la ushindani, Cabanas ana abiria asiyetakikana mwilini mwake - Risasi aliyopigwa bado ipo kichwani mwake na mpira mmoja tu wa kichwa unaweza kumuua. Hii ndio story ya kusisimua mshambuliaji huyu wa kiparaguay.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Salvador Cabanas anapokea pasi  wakati wa mazoezi ya soka na klabu ya daraja la 3 ya Paraguay De Octubre, anageuka na mpira katikati ya sita ya adui na kumpa pasi mchezaji Marcos Gamarra mwenzie na anafunga bao.

Inaweza kuonekana kama ni kitu cha ajabu sana, lakini ndio ukweli uliotokea kama miujiza. Mwezi wa kwanza mwaka 2010, Cabanas aliachwa kwenye sakafu ya Bar ya Mexico City akiwa na risasi iliyozama kwenye ubongo wake.

Kwa kipindi hicho alikuwa kwenye kiwango kikubwa sana cha kucheza soka, akicheza kwenye klabu ya Club America, moja ya timu kubwa sana nchini Mexico, na alikuwa ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi kwenye fainali ya kufuzu michuano ya kombe la dunia 2010 akiwa na kikosi cha Paraguay.

Tembea kwenye mitaa ya mji mkuu wa Paraguay Asuncion, Cabanas alikuwa akipendwa sana na kuheshimiwa kama mchezaji muhimu kwa taifa hilo la Amerika ya kusini kuelekea kwenye WOZA 2010 - lakini ukiwa umebaki muda mfupi kabla ya michuano ya kombe la dunia, Waparaguay wote walikuwa wanajua mfungaji bora wao  hatakuwepo kwenye ndege itakayoipeleka timu South Africa. Hakukuwa na namna angeweza kupona kutoka na ajali ile ya kupigwa risasi ya ubongo huku wakiambiwa na wataalamu kwamba Cabanas ana asilimia 5 tu ya kuwa hai.

Baadhi ya washabiki wa Cabanas wakiwa nje ya Hospitali wakimuombea afya njema kipenzi chao
"Wapasuaji waliniambia ilikuwa ni miujiza kwamba sikufa," Cabanas analiambia jarida la Lence.Lakini kufuatiwa upasuaji aliofanyiwa  na matibabu ya miaka miwili jijini Buenos Aires, amerudi tena kwenye soka mwezi wa nne mwaka huu akiwa na klabu yake ya mtaani kwao aliokuwa nayo, iliopo eneo la Itaugua, mji wenye watu takribani 100,000 - nje kidogo ya mji mkuu wa Paraguay.

Cabanas anajituma bila kuchoka mazoezini ili aweze kurejea kucheza soka la kiushindani, na amekuwa akifanya hivyo kwa takribani miezi minne ili aweze kumpa uhakika kocha wa klabu hiyo ya 12 de Octubre - Rolando Chilavert, lakini kumbukumbu ya tukio la usiku ule kwenye bar ya Mexico City hazitotoka kichwani mwa mshambuliaji huyu: "Nakumbuka vizuri sana, nilienda chooni na aliyekuja kunishambulia akaja kusimama karibu na mie, akanigeukia na kuichukua bastola yake kutoka kwenye suruali yake ya jinzi na akaninyooshea kwenye paji langu la uso.
     "Akaniambia: "Unadhani wewe ni nani? Unajiona wewe ni bora kuliko wengine wote, lakini yote unayofanya ni kucheza soka tu," Nikamjibu nikweli mie ni mcheza soka tu na sio mtu bora kuliko wengine. Akaniambia nilikuwa nawadhulumu Wamexico. 'Sipo hapa kumdhulumu mtu; nikamjibu. 'Nilikuja hapa ili kuweza kufanya kazi yangu ya kucheza soka na kupata fedha zangu halali pamoja na kuisadia klabu yangu  Club America.'

"Baada ya hapo akaniambia kwamba ananiua. 'Nakupiga risasi,' nikamjibu "Endelea tu na unipige.' na kweli akanipiga ."


Risasi ile ikakiingia mpaka kwenye fuvu la Cabanas  na kwenda mpaka kwenye Ubongo wa nyuma wa kichwa chake. Polisi baadae wakampata mpiga risasi ambaye alitambulika kwa majina ya Jorge Balderas, jambazi ambalo linafanya kazi kwa Edgar Valdez Villareal anayejulikana kwa jina maarufu la 'Barbie', mmoja ya wauza madawa ya kulevya wakubwa nchini Mexico.

Mexico imekuwa ikiandamwa na mauaji tangu Raisi Felipe Calderon alipotangaza vita na wa wauza unga mwaka 2006. Zaidi ya watu 50,000 wameuwawa ndani ya kipindi cha miaka 6, kutokana na vita ya magege ya wauzaji unga kugombea maeneo ya uuzaji wa biashara zao huku serikali ya nchi ikitumia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kujaribu kupambana nao.

Maiti 9 zinaning'inia kwenye daraja la Monterrey, vichwa vya watu vilikutwa vikiwa kwenye ufukwe wa Acapulco, maiti nyingine 35 zilikutwa zimetupwa kwenye barabara ya Veracruz - Ilibaki kidogo tu Cabanas aingie kwenye orodha ya wahanga wa vita hii.

"Risasi ipo kwenye mshipa mkuu kichwani," anasema Cabanas. "Mpasuaji hakutaka kuindoa kwasababu ni hatari sana kuigusa. Lakini kitu kizuri ni kwamba walisafisha kila kitu.
"Haiwezekani kupata suluhisho juu ya vita dhidi ya madawa ya kulevya. Wapo mafia wengi sana na kuna mahitaji makubwa kutoka USA kwenye mipaka ya nchi hizi mbili."


Nchi mojawapo ambayo iliweza kupambana na vita dhidi ya madawa na vurugu zake ni Colombia. Kwenye miaka 1980 na 90, nchi hiyo ilikuwa ndio sehemu inayopendwa zaidi na wauza madawa ya kulevya ambao waliyachukua maisha ya mcheza soka Andres Escobar, miongoni mwa wahanga wa wauza madawa hao.

Escobar, akiwa na miaka 27 wakati alipouliwa, alijifunga goli katika michuano ya kombe la dunia 1994 dhidi ya USA, na Colombia wakapoteza mechi na kutolewa kwenye hatua ya makundi.

Wauza madawa, inaaminika waliweka fedha nyingi kwenye kamari kwa ajili ya timu ya taifa ya Colombia kufanya vizuri, hivyo walihakikisha Escobar analipa kwa kuwapotezea fedha zao na wakamuua. Mazishi ya Escobar yaliudhuriwa na watu wapatao 120,000.


ITAENDELEA KESHO - www.shaffihdauda.com



By Aidan Charlie Seif

No comments:

Post a Comment