Search This Blog

Wednesday, November 7, 2012

ADRIANO ATEMWA TENA NA FLAMENGO BAADA YA KUKATAA KURUDI UWANJANI MWAKA HUU

Mkurugenzi wa Flamengo Zinho amesema kwamba klabu hiyo ya Brazil haina mpango kumsaini upya Adriano wakati mshambuliaji huyo wa kibrazil atakaporudi uwanjani mwaka 2013.

Zinho alisema jana Jumanne itakuwa ngumu sana kwa klabu hiyo kumrudisha Adriano mara baada ya mapema leo baada ya mchezaji kutangaza kwamba hatorudi uwanjani mpaka mwakani.
 Mkurugenzi huyo alisema hataacha kujaribu kumsaidia  Adriano mwenye miaka 30 kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika maisha yake binafsi, lakini kikazi amenawa mikono yake na kufikia kikomo.

Akiwa anasumbuliwa na matatizo ya nje ya uwanja kwa muda mrefu, Adriano aliacha kufanya mazoezi mara nyingi tangu alipojiunga na Flamengo mwezi wa August baada ya kufukuzwa na Corinthians kwa kutokuwa makini na kujitunza juu ya majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Adriano amesema uamuzi wa kutocheza mwaka huu ni mzuri kwa kw na klabu pia. 

No comments:

Post a Comment