Search This Blog

Tuesday, October 2, 2012

TIHANA NEMCIC - MSICHANA WA MIAKA MIAKA 24 ANAYEFUNDISHA TIMU YA SOKA YA WANAUME CROATIA



Tihana Nemcic anataka kuheshimiwa kama ilivyo kwa kocha yoyote mkuu kwenye timu ya soka.

Kocha huyo msichana mwenye miaka 24, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake na huku akiwa mwanamitindo, anaonekana sasa kupendwa sana na vyombo vya habari, kwasababu ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya  wanaume ya nchi hiyo inayoshiriki ligi ya daraja la 5 NK Viktorija Vojakovac.

Nemcic, alimaliza masomo yake ya ukocha katika chuo kikuu cha michezo cha nchi hiyo na tangu amechukua majukumu ya kuifundisha klabu ya wanaume amekuwa akisisitiza awe anaheshimiwa na kuonekana kama makocha wengine wanaume hivyo aachwe afanye kazi yake vizuri.

"Mimi ndio kocha mkuu na nina mamlaka yote kutengeneza na kupanga mipango yote ya ufundi wa timu," Nemcic alisema. "Kama mwanamke na mwanaume wote na wana sifa sawa  katika kazi ya ukocha, sioni tatizo lolote kwanini nisiingie kwenye soka la wanaume."

Timu yake kwa sasa inashika nafasi ya 8 katika ya timu 16 za ligi, akiwa na pointi 4, baada ya kushinda mechi moja, kufungwa moja na kutoa suluhu moja..

Tihomir Jagusic, mmoja wa wachezaji bora wa klabu hiyo, anamuelezea Nemcic kama kocha mzuri sana, mwenye mipango thabiti na mtu makini sana katika kufuatiliwa mazoezi ya timu yake.

Nemcic alianza kupenda sana mchezo wa soka wakati alipokuwa akimfuata mpenzi wake mazoezini.

"Nilikuwa naenda kumuangalia anavyocheza, jinsi alivyocheza . . . . . na hapo ndipo na mimi nilipoanza kucheza mwenyewe na soka ikaniingia na kuwa sehemu ya maisha yangu," anasema msichana huyo. "Hii ni changamoto kubwa kwangu. Nimekuwa nikipata uzoefu kufundisha watoto lakini kufundisha timu ya wanaume bado ni changamoto kubwa."  

Nemcic alipokuwa akiichezea Croatia.
Nemcic anasema anaona maisha yake ya siku za uchezaji ni tofauti kabisa na siku za ukocha.

"Unapokuwa mchezaji, unakuwa unajifikiria wewe na kiwango chako tu binafsi," anasema.
"Sasa, nikiwa kocha, natakiwa kuanza kufikiria kuhusu wachezaji zaidi. Lakini kazi zote ni sawa. Zote zina kupanda na kushuka."

 "Tuna sheria," anasema. "Wachezaji wangu wanapoenda kubadilishia nguo, mie huwa nasubiri nje, wanapomaliza mmoja anatoka na kuja kuniita niingie ndani. Sitoweza kujiweka kwenye hali ya kuweza kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo niwakute wakiwa hawapo vizuri kimavazi."

1 comment:

  1. Ana bahati kweli! angefundisha timu ya kina John Terry yangemukuta!

    ReplyDelete