Search This Blog

Thursday, October 18, 2012

MDENMARK MWENYE ASILI YA TANZANIA PATRICK MTILIGA APIGWA MARUFUKU TIMU YA TAIFA YA NCHI HIYO KWA UTOVU WA NIDHAMU

Beki wa Kimataifa wa Denmark, Patrick Mtiliga, mwenye asili ya Tanzania ameambiwa hataichezea Timu ya Taifa tena baada ya kugoma kucheza Mechi  ya juzi ya Nchi hiyo ambayo Denmark ilichapwa 3-1 na Italy kwenye Mechi ya Kombe la Dunia.
Kocha wa Denmark, Morten Olsen, alisema Beki huyo awali alijulishwa atakuwa Benchi na Simon Poulsen ataanza badala yake lakini, wakati wachezaji wanapasha viungo moto kabla mechi kuanza huko jijini Milan, Poulsen aliumia na Mtiliga akajulishwa atacheza mechi hiyo lakini akagoma.
Olsena amesema: “Nipo kwenye Soka kwa Miaka 40 sasa lakini sijashuhudia kitu kama hiki. Amewaangusha wenzake!”
Olsen aliongeza: “Nilimwambia Patrick apashe lakini alikuwa amehuzunika baada ya kwanza kuambiwa hachezi mechi hiyo atakuwa benchi na akasema hawezi kucheza. Hapo ndipo nikamwambia aondoke kwenye kikosi changuna hiyo ndio ilikuwa mechi yake ya mwisho kucheza wakati mimi nikiwa mwalaimu wa hii timu."
 Mtiliga ambaye alikuwepo katika kikosi cha Denmark kilichoshiriki kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2010, pia mwanzoni alikuwa akiichezea klabu ya Malaga ya Spain kabla ya kuhamia timu ya FC Nordsjaelland.

1 comment:

  1. shafii mwambieni arudi nyumbani kwao, maana hat sie atatusaidia, tuna watafuta watu kama hao kwa mema na si kwa utovu wa nidhamu. aje aokoe jahazi maana akina Canavaro, nsajigwa na yondani kama vile wanaelemewa sana na mtiti wa timiu za nchi nyingine jamani, mwiteni kwao

    ReplyDelete