Search This Blog

Friday, October 5, 2012

MAONI YA MDAU JUU YA MAPATO YA MECHI YA SIMBA NA YANGA

1. Juzi nilikuweka kwenye uzi nikikuomba usaidie kuibua hoja ya timu zetu kubwa kuwasajili na kuwatumia wachezaji wa ndani, badala ya wachezaji wa nje ambao kimsingi wana umri mkubwa na hawana value wanayo-add kwenye timu zao husika.
Mfano ni te likes of Kago, Ochieng etc

2. Jana tena, kumeibuka kiroja. Mapato ya Simba ya Yanga kuwa 390m tu. Ni kiroja kwa kuwa, kwa mujibu wa matangazo ya Supersport, mashabiki walioingia ni 59,000. Sina haja ya ku-validate idadi hii, maana kule orange straight nilipokaa, mashabiki walikuwa wamejazana hadi kubebana na kukaa kwenye njia za kuingilia.

Embu tufanye scenario zifuatazo kwa kuzingatia viwango vya viingilio:
- 59, 000 x 30, 000 = 1, 770, 000
- 59, 000 x 20, 000 = 1, 180, 000
- 59, 000 x 15, 000 = 885, 000, 000
- 59, 000 x 10, 000 = 590, 000,000
- 59, 000 x 7, 000 = 413, 000, 000
- 59, 000 x 5, 000. = 295, 000, 000

Hapa mtaona kwamba, tukifanya average (mliosoma hesabu na uhasibu ndo mahali penu hapa), basi walau kiingilio cha 10,000 ndo muafaka ya kuchukuliwa kama waliingia watu wote, mtaona kuwa mapato yalitakiwa yawe, walau 500, 000, 000.

Shaffih, mna deni kubwa sana kwa watanzania katika kuwaeleza, kuwafahamisha na kuwasaidia watanzania ili waepukane na taabu na masumbufu haya wanayoyapata.

4 comments:

  1. Umefanya hesabu za kitoto sana,kumbuka 59 umezidisha kila sehemu wakati sio kweli,unataka kutuambia Vip B kuna viti 59,000?

    ReplyDelete
  2. Mdau nakuunga mkono it is true that what are you saying....TFF wanatakiwa muongozo juu ya hili....Pia kwa ndugu zangu wa Supersport tunawashukuru kwa hili maana mnatuonyesha dhahiri Timu zetu zinavyonyonywa.Kiukweli si Haki nasitaki amini pato liliotajwa....ANGALIZO...uchelewi sikia Supersport haionyeshi tena either match ama idadi ya washabiki kwa match....TFF naomba majibu mdau nakupongeza kwa hili...ni mimi mwenye nia yakuona wachezaji na timu zetu zinapata haki zao toka Mbeya(Yahya Omari)

    ReplyDelete
  3. Hesabu zako hazijakidhi kigezo hata kimoja cha kumshawishi mtu aone usahihi wako. Ilibidi ujue kwanza kila kundi ulilopigia hesabu zako lina seats ngapi. sio unakurupuka tu.

    ReplyDelete
  4. dah mtoa comment uliyetangulia vipi tena!! Nashauri kitu kama hujaelewa usikurupuke kaka!! Rudia tena kwa umakini nadhani utaelewa jamaa alimaanisha nini kwenye hizo average

    ReplyDelete