Search This Blog

Monday, October 8, 2012

AMRI KIEMBA BAADA YA KUIPIGA YANGA - AONGOZA MAUAJI DHIDI YA OLJORO - SIMBA WAKIWATAFUNA WANAJESHI 4-1


Mchezaji wa timu ya Simba Christopher Edward akijaribu kuwania mpira miguuni mwa mchezaji Nafo Zuberi wa JKT Oljoro ya Arusha katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, mpira umekwisha na timu ya Simba imeshinda magoli 4-1 baada ya kuizidi ujanja JKT Oljoro ya Arusha na kutumia makosa ya wachezaji wa timu hiyo, magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Amri Kiemba magoli mwili, Felix Sunzu kwa njia ya penati na Emmanuel Okwi goli moja.
Ni kipindi cha mapumziko wachezaji wa JKT Oljoro wakisali, huku wenzao wa timu ya Simba wakiondoka uwanjani wakati wa mchezo wao wa ligi kuu ya Vodacom leo.
Wachezaji wa timu ya Simba wakiondoka uwanjani mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo huku Simba ikiwa inaongoza kwa magoli 2-1 dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha.

Kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto akikwaana na Markus Raphael wa JKT Oljoro katika mchezo waligi kuu uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam


Mlinzi wa Simba Nasoro Masoud Cholo akigombea mpira na Salim Mbonde wa JKT Oljoro kwenye mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanaj wa Taifa jijini Dar es Salaam leo

Mlinda mlango wa JKT Oljoro Shaibu Issa akikamata mpira mbele ya washambuliaji wa Simba imeshinda bao4-1 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa leo


Mlinda mlango wa JKT Oljoro Shaibu Issa akikamata mpira mbele ya washambuliaji wa Simba.matokeo simba  imeshinda bao4-1. Picha kwa hisani ya Fullshangweblog na mzukakamili-mzuka.blogspot.com

No comments:

Post a Comment