Search This Blog

Friday, September 7, 2012

WAKALA: DEL PIERO AMEKATAA KUJIUNGA NA LIVERPOOL KWA SABABU YA JANGA LA HEYSEL

Wakala wa mchezaji wa zamani wa Juventus gwiji Alessandro De Piero amesema kuwa alikataa kujiunga na Liverpool kwa sababu ya tukio la lilotokea kwenye uwanja wa Heysel kwenye fainali ya kombe la UEFA kati ya Liverpool na Juventus - ambapo mashabiki 36 wa Juve na sita wa 6 Liverpool walifariki huku 600 wakijeruhiwa.

Del Piero amejiunga na klabu ya ligi kuu ya Australia ya Sydney FC jana Jumatano, huku akikataa ofa kutoka Liverpool.

"Nadhani kama Juventino (shabiki wa dhati wa Juve), kwa heshima na kumbukumbu ya mauaji ya Heysel, alikataa kujiunga na Liverpool," Claudio Pasquialin ameuambia mtandao wa TuttoMercatoWeb.


Lakini kwa upande mwingine mchezaji mwenyewe alitoa kauli kwamba amechagua kujiunga na Sydney FC kwa sababu anataka kitu tofauti kwenye soka.

"Niliposema kuna klabu ambazo sikuwahi kuzifikiria  zilionyesha kutaka kunisaini, nilikuwa naizungumzia Liverpool pia," anasema Del Piero. "Nilihitaji kitu tofauti katika kila hali. Ni kweli kwamba Premier league imekuwa ndio ndoto ya wachezaji wengi wa soka duniani.......... lakini mie nilitaka kitu tofauti. Ilibaki kidogo tu niende England lakini nilihisi nataka kitu tofauti." - alimaliza Del Piero ambaye amekuwa na Juventus tangu alipoanza kucheza soka la hadhi ya juu.
                                                                                                             

No comments:

Post a Comment