Search This Blog

Sunday, September 16, 2012

CLOUDS MEDIA GROUP YATOA MISAADA MKOANI DODOMA!

 
Uongozi wa kampuni ya Clouds Media Group,Wasaniii wa muziki wa kizazi kipya na filamu,mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,walezi sambamba na watoto wa kituo hicho wakiwa katika picha pamoja.
Baadhi ya vijana walioko kwenye mafunzo ya kujitolea kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya kituo hicho cha matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma. 
Uongozi wa Clouds Media Group kwa kushirikiana na Baadhi ya wasanii wanaotumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakikabidhi sehemu ya misaada mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo cha The Village of Hope,kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma,kutoka kulia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Shetta,Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simalenga,mmoja wa walezi wa kituo hicho,Sister Maria Rosaria sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Benjamin Gembe wakiwa na watoto wa kituo hicho cha The Village of Hope baada ya kukabidhiwa msaada huo ambao walifurahia kuwa kiasi kikubwa.
Wasanii wa Bongofleva na wasanii wa Filamu kwa pamoja wakifurahi na watoto hao waishio katika mazingira magumu ndani ya kituo cha The Village Hope,chenye jumla ya watoto zaidi ya 180 na idadi ya familia 14
 Baadhi ya walezi wa watoto wa kituo hicho wakishuhudia tukio la kukabidhi msaada huo kwa uongozi wa kituo cha The Village of Hope.
Baadhi ya vijana walioko kwenye mafunzo mbalimbali ya kujitolea wakisaidia kubeba baadhi ya misaada iliyotolewa na Kampuni ya Clouds Media Group ikishirikiana na Wasanii wa bongofleva na wa Filamu.
Mmoja wa wasimamizi wa kituo cha The Village of Hope,Father Vincent Boselli akitoa ufafanuzi mfupi wa mambo mbalimbali ya kituo hicho mbele ya Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Gembe sambana na wasanii wa muziki wa bongofleva na wa Filamu
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Diamond akijitambulisha mbele ya watoto na pia aliwaimbia baadhi ya nyimbo zake na kuwafanya watoto hao wafurahi zaidi,kwani walikuwa wakimuona tu kwenye luninga ama kuzisikia nyimbo zake kwenye redio.
Mmoja wa waigizaji mahiri katika tasnia ya Filamu hapa nchini,Aunt Ezekiel akiwasalimia watoto,kulia kwake ni msaani mkongwe wa bongoflea,Sir Juma Nature akifuatilia kwa umakini tukio hilo adhimu kabisa.
Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akizungumza machache mbele ya uongozi wa kituo hicho.Kulia ni Ofisa wa Maendeleo ya jamii ya manispaa ya Dodoma,Bi.Holda Mwassa,Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Gembe ,Msanii wa bongofleva,Shetta,Pamoja na walezi wakuu wa kituo cha The Village of Hope.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini,Mh Lephy Gembe akiushukuru uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group pamoja na wasanii kwa kuwa na moyo wa kujitolea katika suala zima la kuisadia sehemu ya jamii isiyojiweza.
Pichani juu ni baadhi ya wasanii wa muziki wa bongofleva na Filamu wakisikiliza kwa makini sehemu ya historia fupi ya kituo hicho iliyokuwa ikitolewa na Wasimamizi wa kituo hicho (hawapo pichani).
Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Bwa.Simalenga akizungumza na Wasimamizi wakuu wa kituo hicho cha The Village of Hope kabla ya kukabidhi sehemu ya msaada iliyowasilisha kwenye kituo hicho chenye zaidi ya watoto 180 waishio katika mazingira magumu,ambapo kwa mujibu wa Wasimamizi wa kituo hicho walieleza kuwa watoto wanaowalea ni wale wanaotoka mikoa ya Singida,Dodoma na Morogoro na mikoa ya jirani.
Mkuu wa Vipindi na Utafiti Clouds Media Group,Bwa.Ruge Mutahaba akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mjini,Mh.Lephy Gembe ndani ya kituo cha The Village of Hope,kulia kwake ni Stuwart akiwakilisha sehemu ya Bongo Movie.
Baadhi ya wasanii mbalimbali wakiwasili kwenye kituo cha The Village of Hope,kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment