Search This Blog

Saturday, September 8, 2012

SIRI YA NAPOLI KUTOKUWA NA MAJERUHI WENGI KWENYE KIKOSI CHAO - NI SHERIA YA KUKATA TENDO LA NDOA KWA WACHEZAJI

Timu za soka siku zote zinatafuta njia mpya za kuzuia au kupunguza namba za majeruhi kwenye timu zao ambazo haziepukiki kila msimu na Napoli wameweka sheria moja ambayo ni mahususi kupunguza majeruhi wa misuli. Hakuna kufanya tendo la ndoa siku mbili kabla ya mechi.

Kwa mujibu wa Football Italia

"Kutofanya tendo la ndoa siku mbili kabla ya mechi njia nzuri ya kuzuia maumivu ya misuli," Proffesa Alfonso De Nicola ambaye ni daktari mkuu wa Napoli ameliambia gazeti la Corriere del Mezzogiorno.

"Ni sheria ya kikosi chetu. Pia kuna kazi maalum inayofanywa na wafanyazi walio chini yangu na kocha wa fitness ambayo inalenga zaidi katika kuzuia kuliko kutibu."

Kutokana na njia hii inaoneka kuwa nzuri kwa Napoli, kwa sababu timu hiyo imekuwa namba ya chini ya majeruhi wa misuli kwenye kikosi, lakini taarifa zinasema wachezaji wanaona sheria hiyo ni kali dhidi yao na inawakera wachezaji matajiri.

No comments:

Post a Comment