Search This Blog

Sunday, September 16, 2012

SIMBA NA LYON ZAINGIZA MIL 67/- JKT NA RUVU SHOOTING WAINGIZA LAKI 3 - TIMU ZAGAWANA 29,000


Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.
 
Washabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.
 
Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.
 
Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.
 
112 WASHUHUDIA MECHI YA JKT RUVU v RUVU SHOOTING
Watazamaji 112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
 
Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 10,000 ni 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.
 
Kamati ya Ligi sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,928.78, gharama za mchezo sh. 9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.

1 comment:

  1. ndio maana club zinztzkiwa kuwa na viwanja vyao,umeona kama chamanzi maandaliz ya uwanja yameshinda mgawanyo wa kila timu,aibu na fedhea timu kuondoka na elfu 30,maendeleo ya michezo tzia yana safari ndefu sana

    ReplyDelete