Search This Blog

Friday, September 28, 2012

SIMBA MPENI NAFASI HUYU KINDA: ANAWEZA KUZIBA PENGO LA OKWI DHIDI YA YANGA


Wakati joto la pambano la kwanza la ligi la watani wa jadi Simba na Yanga likizidi kupamba moto, huku Simba wakiwa na pengo kubwa la kumkosa mshambuliaji wao tegemeo Emmanuel Okwi ambaye ana adhabu ya kufungiwa mechi tatu - mashabiki na wanachama wa klabu hiyo pamoja na benchi la ufundi la Simba hawapaswi kuwa fikra kubwa kuhusu pengo la Okwi.

Bahati nzuri ni kwamba Simba walijitahidi kufanya usajili mzuri kwenye safu ya ushambuliaji msimu huu hivyo wapo baadhi ya wachezaji ambao wanaweza kucheza vizuri na kuziba pengo la Okwi. Mmoja ya wachezaji hao ni kinda huyu aliyepandishwa kutoka Simba B iliyochukua ubingwa wa BancABC Super8 anayeitwa Haruni Athumani Chanongo.

Kijana huyu mwenye miaka 20, alikuwa ni mmoja ya wachezaji waliong'ara vilivyo katika michuano hiyo ya Super8, akizisumbua vilivyo ngome za vilabu vya ligi kuu vya Azam na Mtibwa katika mechi za nusu fainali na fainali huku akiwa mmoja ya wafungaji wazuri.

Staili ya uchezaji ya kinda huyu haitofautiani sana na ya Okwi, ana kasi na ujuzi wa kupiga vyenga. Anajiamini na ana uwezo wa kupambana katika kuisadia Simba kipindi hiki ikiwa na pengo la mshambuliaji tegemeo Okwi.


Haruni ambaye mwanzoni alishawahi kuichezea Polisi Dodoma katika ligi kuu chini kocha Sekilojo Chambua, tayari ana uzoefu wa kucheza mechi kubwa na kupafomu vizuri. Hapa anaelezea:
 "Nilipokuwa na umri wa miaka 18 nikiwa na timu ya Polisi Dodoma,kocha Sekilojo Chambua alinipa nafasi ya kucheza mchezo wangu wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom. Nafasi hii ilitokea baada ya baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kuondoka kutokana na timu kuwa na matokeo mabaya,mchezo wangu wa kwanza ulikua dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri uliomalizika kwa sare ya bao 1:1.
Nikiwa na Polisi pia nilifanikiwa kucheza michezo dhidi ya Simba na Yanga iliyomalizika kwa timu yetu kufungwa mechi zote mbili mabao 2:0."

Kwa mujibu wa makocha ambao tayari wameshamfundisha kinda huyu wanasema Haruni ana uwezo mkubwa na anaweza kucheza vizuri kwenye yoyote kwa sababu ana uwezo na anajiamini.

5 comments:

  1. judging from the video i agree with you,he is a decent prospect looks positive on the ball,comfortable in dribbling and always looks to take on defenders.Simba should give chance to this guy plus c.edward and 1 or 2 more players from their Simba B squad.These guy re the future of Simba if we dont appreciate and value them now not only Simba but also Tanzania will loose a great deal of talent.What tanzania especially our football development need is Arsene Wenger like managers someone with philosophy to develop,nourish and give opportunity to world class players which am sure we have.

    ReplyDelete
  2. huyu dogo ni noma simba wanalazmika kuumpa nafasi yani hii simba B kwa ujumla ni kali kuliko ya wakubwa,ya nini kupoteza pesa hali ya kuwa tuna vipaji kama hivi.

    ReplyDelete
  3. aisee huyu dogo ni zaidi ya okwi ana mabo mazuri sana,lazma klabu yetu impe nafasi huyu dogo,kumbe wachezaji tunao cjui klabu yetu inataka nini,huyo ni zaid hata ya samata

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. nilicho gundua watu mnapenda sana kutamka...nilisema mie. hivi unadhani asiyejua umuhimu wa haruni ni nani, hapa simba kila mmoja anajua uwezo wa harun na kipaji cha kipekee ila hii ni team na ina mwalimu tena si wakubahatisha na ndiye alipendekeza waliotakiwa kupandishwa tim A.

    so pia kama tim ina malengo yake na mifumo iliyowekwa so hakuna mtu toka nje ya club yenye wanachama na wapenzi wenye moyo wa dhati na tim yao ajeingilia mambo yasiyo muhusu kwa kutaka kutafuta umaarufu wa kujifanya nyie ndio mliogundua au kusaidia uwezo wa mchezaji flani kwa kusema eti mpeni huyu nafasi atawasaidia..
    tunalijua hilo na tuna vijana wengi wenye uwezo wakuisaidia simba na utafika muda wataonesha uwezo wao na hili wala halipingiki ila hatu weki attention kwaajili ya mechi ya yanga pekee

    hivyo mkiwa mnataka kuandika mambo yahusuyo club hii ni bora muulize ndani ya club kuliko kukurupuka mana tukiwauliza mara ya mwisho kumuona haruna akichezea simba ni lini, najua mtasema ilikuwa super 8

    there's no prediction football in simba n we try our best to make this guys in moldem football kuisaidia simba kwa vipindi vilefu zaidi,,

    hii tuna fananisha maneno yenu kama uchochezi ili mje kusema,, Yulisema sisi wangemchezesha fulani wasingefungwa. acheni kubabaisha fuatilieni mambo kwa kina lol.

    ReplyDelete