Search This Blog

Thursday, September 27, 2012

OFFICIAL: JOHN TERRY AADHIBIWA MECHI NA FAINI YA £220,000 - KUZIKOSA MAN UNITED NA ARSENAL

John Terry ameadhibiwa na chama cha kandanda cha England, FA, asicheze mechi nne, na vile vile alipe faini ya pauni 220,000, kutokana na matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand.

Chama cha FA kilithibitisha Terry alifanya makosa hayo, baada ya kusikiliza kesi dhidi yake kwa kipindi cha siku nne.

Msemaji wa John Terry alisema mchezaji huyo "alisikitishwa" na hatua ya FA, kwa kuamua tofauti, kinyume na mahakama, ambayo awali ilisema hana makosa.

Mwezi Julai, mahakama ya Westminster mjini London ilipitisha uamuzi kwamba mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 31, hakufanya kosa hilo, la kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Ferdinand.

Hata hivyo wengi watajiuliza kwa nini adhabu dhidi ya Terry ni nyepesi mno, ikilinganishwa na ile iliyopitishwa dhdi ya mchezaji wa Liverpool, Luis Suarez mwaka jana.

Terry ana muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, mara tu atakapopokea maelezo ya adhabu hiyo kupitia maandishi.

Adhabu hiyo haitatekelezwa hadi Terry atakapopata nafasi ya kuamua atafanya nini.

Taarifa kutoka klabu yake ya Chelsea iliongezea: "Klabu ya Chelsea inafahamu vyema uamuzi uliopitishwa, na inaheshimu uamuzi huo uliotolewa leo na chama cha FA kumhusu John Terry." 


Kutokana na adhabu hiyo John Terry atazikosa mechi nne zilizo chini ya FA, ikiwemo mechi dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London Arsenal na Spurs pamoja na Norwich na Manchester United.

No comments:

Post a Comment