Search This Blog

Friday, September 14, 2012

'MESSI NA HIGUAIN WANA TABIA ZA KIKE UWANJANI" - ZAMBRANO

Peru walilazimisha sare ya 1-1 na Argentina katika mechi yao ya kufuzu kombe la dunia usiku wa jumanne, lakini mfungaji wa goli la Peru, Carlos  Zambrano, hakuwa ameridhika na matokeo hayo. Pia alizungumzia juu ya tabia za mfungaji wa goli la Argentina. Gonzalo Higuain. Pia alitoa kijembe kwa Leo Messi kwa sababu Zambrano anadhani tabia alizonazo Messi ni za mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 23.

Beki huyo wa Eintracht Frankfurt aliuambia mtandao wa Depor.pe:

"Lionel Messi hakufanya chochote cha maana uwanjani, inawezekana alikuwa anaogopa. Tulikuwa na deni kwa mashabiki wetu na tulilipa deni hilo kwa mpira mzuri. Gonzalo Higuain na Messi  walikuwa wakilalamika kila muda na kila kitu kama wasichana  wadogo. Higuain alijaribu kunipandisha hasira kila muda lakini nilitulia na sikumpa alichotaka.

"Tulistahili kushinda, tulicheza mpira mzuri sana. Nina hasira kwa sababu tulipata pointi moja tu. Tulijua tungeweza kushinda lakini tumepoteza pointi mbili na hilo linatuuma. Waargentina walichanganyikiwa na na hawakujua namna ya kutuzuia. Hawakuweza kumiliki mpira kwa muda mrefu. Walijaribu kutukasirisha kwa kututukana. Walidhani hawawezi kuguswa, lakini hiyo sio sawa kwa sababu mpira ni kwa ajili ya wanaume"

No comments:

Post a Comment