Search This Blog

Saturday, September 8, 2012

MAMBO MANNE MUHIMU KUMUHUSU CRISTIANO RONALDO

> Pamoja na utajiri mkubwa alionao akiwa ndio mcheza soka anayelipwa vizuri zaidi duniani nyuma ya David Beckham kwa mujibu wa jarida la Forbes. Cristiano Ronaldo ni tofauti na vijana wengine wenye mafanikio kama yake - yeye hanywi pombe kabisa. Unajua kwanini?
Baba yake alifariki kutokana na matatizo yaliyosababishwa na unywaji wa pombe. Hivyo Ronaldo hanywi pombe kwa kuwa inamkumbusha kifo cha baba yake.

> Wakati baba yake alipokuwa hai, ndoto yake kubwa ilikuwa ilikuwa ni kumuona mwanae akishinda tuzo ya uchezaji bora wa dunia, na mwaka 2008 akiwa na Manchester United aliitimiza ndoto hiyo ya marehemu baba yake. 

>Tumeshuhudia watu wengi maarufu wenye fedha kama Cristiano Ronaldo wamekuwa wakitumia fedha zao nyingi katika kujichora tatoo, lakini pamoja na ubishoo wote alionao Cristiano Ronaldo anasema hajachora tattoo kwa sababu ana changia damu mara nyingi.

> Ronaldo alitoa kiasi cha €3 Million ambazo ni sawa na fedha za madafu zaidi ya Billion 7 kwa nchi za kiafrika zilizokuwa zinakabiliwa na balaa la njaa.

No comments:

Post a Comment