Search This Blog

Wednesday, September 19, 2012

DROGBA NA ANELKA KUONDOKA CHINA? HATMA YAO KUJULIKANA MWISHO WA MWEZI

Hatma ya wachezaji wawili Didier Drogba na Nicolas Anelka  katika klabu ya Shanghai Shenhua itajulikana mwishoni mwa mwezi huu.

Wachezaji hao wawili wa zamani wa Chelsea wapo katikati ya mgogoro wa fedha unaowahusisha wamiliki wa klabu.

Gazeti la Evening Standard linasema Zhu Jun ametishia kuondoa fedha zake kwenye klabu kama asipopewa nafasi ya kuiendesha klabu mwishoni mwa mwezi huu.

Bila fedha za billionea huyu, Shanghai  hawatoweza kuwalipa Drogba £250,000 kwa wiki na Anelka £200,00.

"Sasa nimefanya maamuzi magumu ya kuwaamini tena, mara miwsho! na safari hii nina deadline ya wiki mbili," aliandika Zhu katika mtandao wa Weibo.

Drogba na Anelka bado wanatakiwa na vilabu kibao vya ulaya, hivi karibuni Drogba akiwa nahusishwa na kurudi jijini London kuichezea Arsenal huku Anelka akiwa na hot cake kwenye vilabu vya katikati mwa ligi.

No comments:

Post a Comment