Search This Blog

Saturday, August 18, 2012

OFFICIAL: BARCELONA NA ARSENAL ZAKUBALINA ADA YA UHAMISHO WA ALEX SONG


Klabu ya FC Barcelona imetangaza jioni hii kwamba imefikia makubaliano juu ya ada ya uhamisho wa kiungo Mcameroon Alexander Song kutoka Arsenal.

Song sasa atasafiri kwenda Barcelona ndani masaa 48 yajayo kwa ajili ya kufanya vipimo na kujadiliana huu ya maslahi binafsi kabla ya kusaini mkataba na Barcelona.

Uhamisho huu wa Song unakuja siku moja baada ya Robin Van Persie kukamilisha uhamisho wa kujiunga Manchester United akitokea Arsenal. Kuondoka kwa Song kunamaanisha Arsenal sasa itakuwa imeuza wachezaji wake muhimu waliocheza kwa kiwango kikubwa msimu uliopita na kuiwezesha kushika nafasi ya 3 kwenye ligi kuu ya England.

Alex Song anakuwa mchezaji wa nne wa Arsenal kujiunga ba Barcelona katika kipindi cha miaka 5 iliyopita, wa kwanza akiwa Thierry Henry, akafuatiwa na Alexander Hleb, Cesc Fabregas na sasa mcameroon huyo.

1 comment:

  1. I was trying to b optimist with Wenger for so long lakini kwa hili la Song wacwac unaanza kuniingia.Unless kuna proper replacement ya Song aliye ktk mipango ya Wenger.Lakini pia huyo atakayekuja itamchukua muda gani kukidhi haja yetu gunners(vikombe)?

    Mie binafsi ctaki yale ya msimu uliopita(Timu kukumbuka shuka kukiwa kumekucha)
    Ifikie wakati mgt ijue timu ina sides tatu(Wachezaji,mgt na Mashabiki)Furaha ya mgt ni sound financial position,ambayo kwetu Gunners tumeijenga vyema kwa miaka kadhaa sasa.Furaha ya wachezaji ni mafanikio(hapa namaanisha vikombe pamoja na malipo mazuri)
    FURAHA YETU MASHABIKI ni vikombe.

    Leo man u,city,Barcelona na Madrid wanaongeza idadi ya mashabiki(asset) c kwa kuuza wachezaji wala kusifika kukuza vipaji tu bali ni mafanikio yao kama timu.Jiulize hizo timu hapo juu zinavuna mashabiki kiasi gani kwa mwaka kule Asia,hapa Africa na hata kwao Ulaya!

    Lazima tuangalie pande zote tatu tunapojenga Arsenal yetu.

    ReplyDelete