Search This Blog

Saturday, August 18, 2012

MABADILIKO YA UONGOZI YANGA YALIVYOCHELEWESHA MCHAKATO WA KAMPUNI YA LIGI KUU (TPL)

Wakati ligi kuu ya Tanzaia bara ikiwa imepangwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo, kumekuwepo  hakuna taarifa yoyote rasmi juu ya muendeshaji wa ligi hiyo kampuni (Tanzania Premium League -TPL) ambayo itakuwa ikiundwa na vilabu vishiriki vya ligi kwa pamoja na TFF kama wenye hisa.

Kama itakumbukwa wakati wa ligi ya msimu uliopita ikiwa imefikia katikati, vilabu vya ligi kuu kwa kushirikiana na wadau tofauti walianzisha harakati za kutaka ligi kuu ya msimu uliopita ngwe ya pili iendeshwe na kampuni ya vilabu vyenyewe na sio TFF kama ilivyo kwenye ligi kuu za Kenya, EPL na nyingine duniani.

Vikaendeshwa vikao na ikaundwa kamati ya kushughulikia mchakato wa uanzishwaji wa kampuni iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Godfrey Nyange Kaburu akisaidiwa na katibu mkuu wa Yanga Celestine Mwesiga na viongozi wengine wa vilabu. Kamati ile ilifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha awamu ya pili ya ligi msimu uliopita inachezwa chini ya TPL, lakini ikaenda na ikaonekana kwamba muda haukuwa sahihi kwa TPL kuichukua ligi katikati mwa msimu, hivyo ikashauriwa na TFF chini ya Leogdar Tenga iundwe kamati ya ligi kuu ambayo ingesimamia ligi kuu kwa nusu ya msimu iliyobakia na kampuni itachukua ligi msimu mpya huu wa 2012-13. Ikaundwa kamati ambayo iliundwa na timu ya viongozi hawa vilabu, Kaburu, Celestine Mwesiga, Meja Charles Mbuge, Said Mohamedi, Seif Ahmed 'Magari', na Henry Kabera.

Ligi ikaisha na mchakato wa kuanzisha Tanzania Premium League - TPL unaendelea vizuri na ilikuwa imebaki tu umoja wa vilabu wakiwakilishwa na kampuni yao  kukutana na shareholder mwingine TFF ili kuweza kuweka sawa mipango na taratibu za miwsho kabla ya mchakato kukamilika.

Ikumbukwe mwanzoni kabisa wakati wa kuanzishwa kwa mchakato wa kuunda kampuni vilabu vilishakubaliana vyote kwa pamoja kwamba wote watakuwa na haki sawa kwenye kampuni hiyo. Lakini hivi karibuni mambo yote yakiwa yapo mwishoni kwa bahati mbaya au nzuri mabingwa wa Kagame Cup wakafanya mapinduzi kwenye safu ya uongozi wa klabu yao, na hatimaye wakapata uongozi mpya chini mwenyekiti Yusuph Manji.

Wakati kikifanyika moja ya vikao vya mwisho, Manji kama mwenyekiti wa Yanga  alipata nafasi ya kuhudhuria kikao kimojawapo na ndipo akaleta hoja mpya ambayo ilishajadiliwa kuhusu mgawanyo wa mapato ya kampuni - akisema haifahamu na kwamba Simba na Yanga ndio vilabu vikubwa na vyenye kuingiza faida nyingi hivyo haviwezi kupata mgawo sawa na vilabu vidogo, akijenga hoja hiyo itakuwa ni kuvionea vilabu vya Simba na Yanga. Matokeo yake viongozi wa vilabu wengine wakapingana nae na wakasema hilo lilishajadiliwa na maamuzi yalishapitishwa chini ya viongozi wawikilishi wa vilabu vya Simba na Yanga - Godfrey Kaburu na Celestine Mwesiga,  hivyo kushindwa kufikia maafikiano na mambo kushindikana kuendelea mbele.

Wakati haya yakiendelea mdhamini anayemaliza muda wake wa udhamini kampuni ya simu ya Vodacom alionyesha nia ya kutaka kusaini mkataba mpya, kupitia mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo ikawasiliana na TFF juu ya kuanza mazungumzo ya mkataba mpya wa udhamini wa ligi, na kwa kuwa TFF yenyewe itaiachia kampuni ya TPL kuendesha ligi kuu hivyo Tenga imebidi aitishe mkutano na viongozi wa vilabu ambao tayari wameshaanza kutokuelewana juu ya maslahi - wakae pamoja ili kuweza kuujadili mkataba mpya na Vodacom kwa ajili ya udhamini wa ligi ya msimu ujao.

6 comments:

  1. Manji yupo right kwani hata EPL Manchester United haiwezi kugawana mapato sawa na QPR.

    ReplyDelete
  2. Angalia spain barca na real ndio wanaochukua mapato makubwa kwa sababu wao ndio wanatengeneza mapato makubwa pia,jiulize simba wakicheza na toto mwanza ni kiasi gani kinapatikana,je ni sawa na toto akicheza na JKT ruvu?jibu hapana,why wazinyonye timu zingine wakati hawazalishi sawa?komaa manji

    ReplyDelete
  3. Manji hayko sahh kwan hao anaoxema n vlab vdogo ndo vnamfanya yy aonekan mkbwa bla wao mapato yako wapi?

    ReplyDelete
  4. Hawagawani mapato sawa yanayotokana na nini? Ishu hapa ni vyanzo vya mapato!

    Uingereza tv revenue haina shida kwani mgawanyo wake ni kutokana na game zinazoonyeshwa...
    League sponsorship wanagawana pasu kwa pasu, hakuna anayechukua zaidi.
    Mapato ya mlangoni ni ya timu mwenyeji, kila mtu ana uwanja wake.

    Sasa wewe shehe hapo juu unazungumzia lipi?

    ReplyDelete
  5. Kwani duniani pote hali ikoje? Akina kaburu walistruggle sana na hili jambo. Kote duniani vilabu vina share sawa na kwa maana ya mapato ya mdhamini vilabu vyote vinapata equal share. Tofauti ya kimapato inapatikana katika tv rights ambapo timu zenye wapenzi wengi na mechi zao kuoneshwa zaidi wanapata mgao mkubwa zaidi. Simba na yanga watapata more kweye gate collections kwenye game zao za nyumbani na merchandise sales. Manji tofautisha biashara ya uraiani na biashara ya mpira. Guys go go go acheni longolongo

    ReplyDelete
  6. Kwa hili nadhani watu wenye ufahamu nalo walifanyie kazi na walitolee ufafanuzi kwa wadau. Sina ufahamu nalo na hivyo nahisi si vema nikafanya hapa ndio pahala pa kuonesha ushabiki wangu. Tukishafahamu wengine wanafanyaje basi tuone katika mazingira ya nchi yetu hili jambo linawezaje kufanyika kwa manufaa ya mpira.

    ReplyDelete