Search This Blog

Wednesday, August 1, 2012

EXCLUSIVE: NGASSA AFUNGUKA: SINA TAARIFA RASMI JUU YA KUUZWA SIMBA - AZAM WAFUATE TARATIBU

Muda mchache uliopita tumefanikiwa kufanya mazungumzo na mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa ambaye klabu yake Azam leo imethibitisha kwamba ameuzwa kwenda klabu ya Simba.

Katika mazungumzo hayo Mrisho Ngassa amesema  kwamba yeye binafsi hajapata taarifa rasmi kutoka kwa klabu yake ya Azam juu ya kuuzwa kwenda Simba. "Kiukweli hizo taarifa mie nazisikia na kusoma kwenye mitandao tofauti lakini muajiri wangu bado hajanipa taarifa rasmi juu ya hili suala. Pia huu utaratibu sidhani kama ni sahihi, wanawezaje kuniuza timu nyingine bila kunihusisha, vipi kuhusu maslahi yangu katika hiyo timu nyingine nani ameyasimamia? Kwa maana hii bado nashindwa kuamini kama Azam watakuwa wamefanya hivyo. Ilipaswa wanipe taarifa kwamba Ngassa tunakuuza kwenda timu fulani na nina haki ya kuchagua kukubali au kukataa.

Ngassa akaendelea alivyoondoka Yanga, "Mimi sitaki kuondoka Azam huku kukiwa kuna hali ya kutokuelewana kati yangu na wao pamoja na wapenzi na mshabiki wa klabu hiyo ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye kipindi chote nilichokaa pale. Unaweza ukajiuliza kwanini mimi mpaka leo kwanini mashabiki wa Yanga wanaonyesha mapenzi kwangu au ninakuwa na ukaribu nao, ni kwa sababu wakati naondoka Yanga nilipewa baraka zote na klabu yangu, yaani niliondoka vizuri. Azam walikuja wakaongea na Yanga wakakubaliana na ada ya uhamisho then na mie nikapewa taarifa nikakaa chini na Azam tukakubalina mahitaji yangu binafsi sasa iweje leo wao wameshindwa kufuata utaratibu ule ule ambao waliufuata wakati wa kuninunua kutoka Yanga. Ilipaswa wao kabla ya kukubaliana na Simba ingebidi na mie nipewe taarifa ili kuweza kukubaliana mahitaji yangu binafsi na Simba then ndio niuzwe. lakini sivyo walivyofanya."

Alipoulizwa kama Simba wakimpa vile anavyovitaka atakuwa tayari kuichezea klabu hiyo, Ngassa alijibu, "Mpira ni kazi yangu, ninafanya hii kazi ili kuweza kujikimu kimaisha maisha. Kama klabu yoyote ikikubali kunipa mahitaji yangu niyatakayo na nikapendezewa nayo nitajiunga nayo. Taratibu lazima zifuatwe na kuniuza kama kiroba cha mchele, kwa hali ilivyo mpaka sasa sitoweza kujiunga na Simba"

By Aidan Charlie

11 comments:

  1. Hapa sheria sijui itakuwaje, kama hakutakuwa na personal contract between Ngassa na simba kutakuwa hakuna mkataba na deal litaharibika. nilizani Azam wapo kivingine kumbe nao wamo humo humo kama vibabu vyetu viwili.acceptance ya offer kwa upande wa mchezaji razima ikubaliwe, wao wangesubiri waone kama timu anayoipenda itapanda dau na sio kuharakisha na labda wangepata zaidi kwa vibabu kugombania. Lakini Mhhhh mapinduzi ya soka yanarudi kinyume nyume......

    ReplyDelete
  2. That simple, azam wakae wakubaliane na ngasa kuhusu simba, na ni vizuri pia simba wakae na ngasa wakubaliane vinginevyo itakuwa ni vurugu nyingine.

    ReplyDelete
  3. Azam ndiyo wale wale,wameona ni vizuri kuwapa ndugu zao Simba,lakini sasa Simba jiulizeni kitu kimoja,mmepewa ngasa bila ya makubaliano naye mwenyewe,je kweli atacheza kwa moyo mmoja? Siku zote Simba mnapenda kukurupuka,yaani ndiyo mfumo wenu kwa nini?
    Hawa Azam nao sifa ya mapinduzi ya soccer imeporomoka,wanaonekana watu wa viigizo,wamejaa majungu tu hawana jipya!

    ReplyDelete
  4. INABID TUFIKE MAHALI TUFATE SHERIA NA MAKUBALIANO HAIWEZEKANI UMUHUZE MCHEZAJI KM KIROBA CHA MCHELE KWA MFUMO HUU WA NGASSA KUUZWA HIVI AZAM FC PMJ NA SIMA SC WAMEKOSEA TENA SN

    ReplyDelete
  5. Nimesikitishwa na hili jambo...Mtazamo wangu nilidhani Azam wamekuja kuleta maendeleo ya Soka kumbe hamna kitu. Mimi sioni sababu ya Mchezaji kuuzwa kama Kiroba..na kama sababu yenyewe ni kuibusu Jezi ya Yanga? Cha msingi ni je mchezaji anadeliver anapokuwa uwanjani? Mtizamo wangu ni kuwa Azam ni kama tawi la Simba....Kwa mtindo huu soka letu halitaendelea na tutabaki na majungu na kutuhumu kuwa wachezaji hawajitumi...na kufukuza makocha kila kukicha. Hii nchi nafikiri imelaaniwa katika kila kitu.

    ReplyDelete
  6. ....kama Azam wana nia ya kumuuza Ngassa wafate taratibu zote,kwanza waongee na Ngassa kama anaridhika na uamuzi wa kuuzwa i.e kama mkataba umeisha anaweza kuongeza ama kutafutiwa timu nyingine inayomtaka na hapo timu inayomtaka ni lazima pia ifate taratibu kwanza kwa kuongea na Azam kukubaliana na pia ngassa mwenyewe kama analidhika na deal vinginevyo mchezaji atakua hakutendewa haki.

    ReplyDelete
  7. Kwani ajabu mtoto kufanana na baba'ke?..Simba na Azam mtu na mwanae

    ReplyDelete
  8. Mbona Ngasa anajichanganya? kwenye post iliyotangulia kwenye hii blog amenukuliwa akisema yuko tayari kucheza popote Azam watakapomuuza na inaonyesha ana taarifa hizo. Mbona haeleweki?

    ReplyDelete
  9. Kiukweli mimi binafsi nilikuwa naamini kwamba Azam wataleta mapinduzi ya soccer lakini kwa hili la Ngassa nimewaskusha hadhi na kuamini kwama wao ni tawi la simba moja kwa moja ila ya kipingamizi.Kwasababu timu kama timu lazima imruhusu mchezaji kwenda timu aitakayo ilimradi vigezo vyote na taratibu zote zimefuatwa,mfano RVP sasa hivi kocha Wenger anajadiliana naye na pia timu anayotaka kwenda pia wanamshawishi na sio kuamua kama Azam walivyokurupuka,jamani soccer la bongo linaelekea wapi?

    ReplyDelete
  10. Hata kama Ngassa amekosea...mchezaji anapaswa aitwe ajieleze na kamati husika inachukua hatua za kisheria na bila upendeleo wala chuki. Inaonekana Azam wamekuwa na JAZBA mno...Kwa mwendo huu..TZ bado tuko mbali sana katika kuelekea kwenye mapinduzi halisi ya kuendeleza soka Tanzania...Hizi sababu zote zinazotolewa sijui tuliweka muda wa timu zinazomtaka zitume maombi...hiyo yote ni danganya toto..niachokiona mimi hapa ni kutaka tu kumkomoa mchezaji kutokana na kitendo chake...hapa sababu inayowaumiza ni kuibusu Jezi ya yanga..ingekuwa jezi ya Mnyama..angeachiwa tu...Acheni Unazi Azam chezeni mpira

    ReplyDelete
  11. Ubabe umezid kwa hawa viongoz wetu wasio jua mpira wanamuonea ngasa coz hayo nimaisha yake busara itumike tuache ushamba

    ReplyDelete