Search This Blog

Saturday, August 18, 2012

EDWARD CHRISTOPHER WA SIMBA B APIGA HAT TRICK FAINALI YA SUPER8 NA KUIBUKA MFUNGAJI BORA

Mshambuliaji wa klabu ya Simba B ambaye msimu ataonekana kwenye ligi kuu ya Tanzania bara, Edward Christopher ameibuka mfungaji bora wa michuano ya BancABC Super8 iliyomalizka leo kwa klabu ya Simba B kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mipya.

Edward ambaye kabla ya mchezo wa leo alikuwa na mabao matano, katika mchezo wa fainali ya leo aliweza kufunga hat-trick na kusiadia timu yake kubeba ubingwa huku yeye mwenye akimaliza akiwa na magoli nane na hivyo kutawazwa kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo ambayo ndio imefanyika kwa mara ya kwanza msimu huu.


2 comments:

  1. Hizo ni changamoto tunatakiwa tulee vipaji vyetu tuache kupoteza hela nyingi kwa kina sunzu!
    R simtanda.

    ReplyDelete
  2. Vichwa vya Rage na Genious Kaburu vigumu sana. Waliopoteza wakati kuandaa hii timu walikuwa na wazo kuwa hii ndio iwe chanzo cha Usajili wa Simba. Watu hawa ni wabishi na wabinafsi kwenye maamuzi na wachonganishi wanaposhindwa. Wa nini Kanu? Wa nini Danny, wa nini lino?? Simba tutapata hasara sana kwa ubishi wa watu hawa.

    ReplyDelete