Search This Blog

Saturday, July 21, 2012

TIMU YA KITUO CHA TSC MWANZA YAENDELEA KUFANYA VIZURI UJERUMANI - YATOKA SARE NA WAPINZANI WA BAYERN - 1860 MUNICH B

Kikosi cha TSC Mwanza kikijifua kabla ya pambano.
Timu U20 ya TSC Sports Academy, leo imeanza mashindano ya Inselcup, katika kundi B kwa kutoka sare ya magoli 2 kwa 2 na timu ngumu kabisa ya 1860 Munich, amboyo ni moja ya tumu bora 5 katika ligi ya vijana ya Ujerumani.
 
 Magoli ya TSC ya lifungwa na Saidi Hassan katika kipindi cha kwanza, na Tito Jonathani aliongeza bao la kuongoza katika kipindi cha pili.
 


Timu  zikiwa zimejipanga uwanjani kuanza mchezo
Katika mchezo huo 1860 Munich ndio walioanza kufunga katika kipindi cha kwanza, dk ya nne ya mchezo na baadae TSC kusawazisha katika dk ya 11 ya kipindi cha kwanza, kipindi cha pili kilipoanza TSC waliongoza bao, na baadae kusawazishwa na timu ya 1860 Munich dk 7 kabla ya mchezo kumalizika. Mchezo huo ulikuwa mgumu kabisa kwa timu zote kushambuliana zamu kwa zamu. 
Kikosi cha 1860 Munic B kikiwa jukwaani kusubiri mechi yao ianze.
Mechi nyingine ya Kundi B ilikuwa kati ya Maccabi Haifa ya Israel (Mabingwa katika logi ya vijana Israel wametoka suluhu ya 1-1 na TSG 1899 Hoffenheim, ambayo pia inacheza ligi ya vijana ujerumani.
Haya ndio makombe wanayogombania
Katika mechi nyingine za kundi A zilizofanyika katika uwanja huo huo wa Mannheim (Uliopo jimbo la Mannheim) hapa Ujerumani,
Timu wenyeji -SV Waldhof Mannheim 07 walifungwa na H.N.K Hajduk Split ya Croation Magoli 2 - 0
Pia katika kundi hilo timu ya........SPVGG 03 Ilvesheim iko katika daraja la chini kabisa ligi ya vijana Ureumani, walifungwa goli 7-0 na timu ya Karlsruher Sports Club ambayo ipo kwenye moja ya nafasi za juu katika ligi ya vijana Ujerumani.

No comments:

Post a Comment