Search This Blog

Friday, July 20, 2012

THIAGO SILVA: MASHABIKI WA AC MILAN SIKUPENDA KUHAMA SAN CIRO ILINIBIDI.

Pale mchezaji ambaye mashabiki wa klabu fulani wanakuwa wana mapenzi nae makubwa na akahama basi ni kawaida sana kusikia akiitwa mroho wa fedha, na maneno mengi ya kejeli. Lakini baada ya kukamilisha uhamisho wake wa kwenda PSG pamoja na Zlatan Ibrahimovic, Thiago Silva ameamua kuweka wazi kwamba hakutaka kuhama Milan na wala hajaenda PSG kwa sababu ya fedha na utajiri wa klabu hiyo.

Silva alikaririwa na FourFourTwo akisema: "Nilikuwa na furaha kwenye uhamisho huu na nilijisikia huzuni kuondoka Milan kwa sababu nilitokea kuipenda sana klabu ile.

"Watu wananiita mroho wa fedha, ambo ambalo linanikera. Sipati fedha nyingi sana hapa PSG. Hili sio kosa langu. Ningependa kuomba samahani kwa mashabiki wa AC Milankwa kuondoka.

"Uhamisho huu ulikuwa mgumu sana kuutekeleza. Sikutaka kuondoka Milan hata familia yangu pia. Lakini lilikuwa jambo chanya kufanya kwa sababu mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo na kocha Carlo Ancelotti waliniita."

No comments:

Post a Comment