Search This Blog

Thursday, July 12, 2012

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA YATWAA UBINGWA WA URAFIKI CUP - YAIFUNGA AZAM KWA PENATI


Felix Sunzu anaipatia Simba bao la kuongoza hapa uwanja wa Taifa kwenye dakika za mwanzo kabisa za mchezo.

Dk ya 45 Azam wanasawazisha goli hapa na mpira unaenda mapumziko matokeo yakiwa sare. Mcha Viali ndio mfungaji wa goli.

Kipindi cha pili kinaanza hapa timu zinashambuliana kwa zamu. 

Azam wanapata bao la pili John Bocco anaweka mpira kimiani.

Simba wanapata penati na Mwinyi Kazimoto anaenda kupiga penati hiyo. 

Ni goli - Mwinyi Kazimoto aka Failasufu anafunga bao la pili kwa upande wa Simba. 

Mpira umeisha na timu zimeanza kwenda kwenye hatua ya penati.

Penati zinamalizika kupigwa na Simba wanatoka na ushindi wa penati 3-1 na matokeo ya jumla yakawa 5-3.

9 comments:

  1. safi sana Shafii sisi mimi nipo nje ya TZ nafuatilia huo mtanande naomba uendelee kutupa updates

    ReplyDelete
  2. umenogewa mbona update hakuna? kimya sana....

    ReplyDelete
  3. dauda unatoa update kimahaba sana

    ReplyDelete
  4. Shafii safi sana tunaomba uwe unasema ni dakika ya ngapi hayo magoli ya pia update mfano ya kila takika 5 tafadhali 2 yana fungwa na

    ReplyDelete
  5. thanks for good news nilikuwa sijajua matoke. simba bingwa.

    ReplyDelete
  6. Mnyama nouma bado anatanua wigo wake ktk tz

    ReplyDelete
  7. asante kaka japo nipo kijijini mwese mkoa wa katavi najenga taifa nakupata vilivyo kupitia blog yako na nijaliwapo wese nakupata kupitia clouds fm the peoples' station ASANTE SANA KWA TAARIFA YA USHINDI WA SIMBA KESHO INABIDI NIUE JOGOO KARIBU

    says reuben(reubenswilla@ymail.com)

    ReplyDelete
  8. simba chama kubwa....hongereni sana simba sehemu ya makombe!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. hongereni watani zetu,naona sasa mnastahili kuitwa wazee wa matuta,maana mlitufunga yanga kwa matuta,wabunge wenu wakatufunga kwa matuta na sasa mmeendeleza fomesheni ya ushindi wa matuta hata kwenye makombe ya mbuzi,kwani jana mlisawazisha kwa tuta la utata na baadae kushinda kwa matuta.hongereni sana mnaweza kuchukua hata kagame kwa matuta.inaonekana milovan ni kocha mzuri wa penati

    ReplyDelete