Search This Blog

Friday, July 27, 2012

KUPORWA KWA MKEWE MNJINI NAPOLI KWAZIDI KUIPA NAFASI CHELSEA KUMSAJILI CAVANI

Edinson Cavani akiwa na mkewe na mtoto wao.
Nafasi ya Chelsea kuweza kumsajili mshambuliaji wa Napoli Edinson Cavan imezidi kuongezeka baada ya mke wa mchezaji huyo kuporwa mapema mchana kweupe katika mitaa ya Naples.

Mke wa Cavan Maria Soledad anasemekana kwamba tukio hilo limempa mshtuko mkubwa na kumkera sana baada ya saa yake aina ya Audemars Piguet, yenye thamani ya £14,500 kuibiwa na wanaume wawili akiwa anatembea kuelekea kwenye gari lake.  Kuporwa kwa mke wa mchezaji huyo kumekuja muda mfupi nyumba ya wanandoa hao kuvamia na wezi.

Kuongeza mafuta kwenye moto, Cavani mwenyewe alikuwa nchini Uingereza akijiandaa na timu yake ya taifa kucheza kwenye Olympic.

Wakala wa Cavani Claudio Annelucci alisema: " Sio wakati mzuri huu, lakini wanajaribu kusahau juu ya matukio haya. Maria ameondoka Naples na kwenda kuungana na mumewe Cavani Uingereza. Ni vigumu kuzoea mazingira ya namna hii kukutokea. Ni kweli matukio ya namna hii yanaweza kumtokea mtu yoyote."

Moja ya vitu vinavyoonekana kuweza kuwa kikwazo kwa mchezaj huyo kutua London ni ada ya uhamisho, huku mmiliki wa Napoli akimuwekea gharama za €100 million Cavan.

No comments:

Post a Comment