Search This Blog

Thursday, July 19, 2012

JAIRZINHO WA SASA NA UBUNIFU WA CRISTIANO RONALDO? NI KITU GANI LUCAS MOURA ATALETA KWENYE KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED

Jumanne jioni klabu ya Sao Paulo ilitangaza imekataa ofa mpya ya tatu kutoka kwa Manchester United kwa ajili ya kumsaini kiungo mshambuliaji Lucas Moura.

Ofa hizo tatu zimekuja kwenye kipindi cha wiki na kuona namna ambavyo United wamekuwa wakimhitaji kinda hilo la kibrazili kwa kutoka kutoa ofa ya €25 mpaka €38 million.

Inaaminika Sao Paulo wanaweza kukubali ada ya uhamisho ambayo itawapatia wao kiasi cha €35 million, watakayopipata katika malipo ya jumla ya mchezaji ambaye wanamiliki asilimia 80% ya haki zakeza kibiashara, kwa maana hiyo ili mchezaji apate asilimia 20 zake kutokana na malipo ya kusajiliwa kwake itabidi United walipe kiasi cha €44 million.

Siku ya Jumanne kuna taarifa zilitoka tena nchini Brazili, zikiripoti kwamba maofisa wa klabu ya Sao tayari wameshaikubali ofa ya United, lakini huku Inter Milan wakiwa nao wapo kwenye mchakato wa kumtaka, raisi wa klabu ya Sao Paulo anajaribu kucheza kamari kuona kama timu hizo mbili za ulaya zitaendelea kumpandia dau kinda lake.

Lakini muda unazidi kwenda.

Mwezi ujao, Sao Paulo watapoteza asilimia 10 kwenye haki za kibiashara za Lucas Moura, hivyo kubakiwa na 70% na kumi zikienda kwa mchezaji mwenyewe hivyo kufikisha 30% kwa mujibu wa mkataba wao.

Ikiwa dili linatakiwa kukamilika then inabidi limalizike mwanzoni mwa August.

Lucas, kwa upande wake ametulia na yupo comfortable pale Morumbi, ambapo anapata £10,000 kwa wiki kwa mazingira ya Brazil.

Kuhamia England au Italy kutamuongezea malipo makubwa bila shaka, lakini mpaka leo bado hajatoa tamko la kutaka kuhamia popote.

Fedha za udhamini na nyingine wanazopata kwenye matangazo ya Televison zinamaanisha Sao Paulo hawapo kwenye uharaka wa kumuuza Moura.

Kama Moura ataendelea kubaki Brazil, kwa hakika ataendelea vizuri na kuhakikisha anapata malipo mara tatu zaidi ya anachokipata sasa baada ya kusaini mkataba mpya na klabu yake.

Kinda la Santos Neymar, kwa mfano, analipwa £90,000 kwa wiki - mshara mkubwa sana kwa kinda la miaka 20 kwa viwango vya ligi yoyote.

Vijana makinda wa kibrazil kwa sasa hawana tena mshawasha wa kuhitaji kwenda kucheza ulaya wakiwa na umri mdogo kwa maana ya kutaka fedha zaidi.

Lucas, kwa bahati nzuri atacheza mechi moja pale Old Trafford pale Brazil itakapokutana na Belarus kwenye mchezo wa group C tarehe 29 mwezi huu kwenye Olympic.

Lakini ili kuweza kuwa na uhakika wa kuendelea kucheza kwenye uwanja huo Lucas itabidi aombe aidha United waongeze ofa kwa mara nyingine tena au Sao Paulo wapunguze bei yake.

Ikiwa United watafanikiwa kumnasa Lucas Moura watakuwa wamejipatia mshambuliaji ambaye anaweza kucheza popote kwenye eneo la ushambuliaji.

Mchezaji aliyekamilika akiwa na nguvu, ujuzi na kasi - ni mchezaji anayeweza kuitingisha ngome yoyote ya ulinzi kwa uwezo na kasi aliyonayo.

Huku akiwa amesememwa ya kuwa na tabia ya ubinfsi kipindi cha nyuma kwa kumiliki sana mpira mwenyewe na kushindwa kuwalisha wachezaji wenzie, lakini pia ana uwezo wa binafsi ambao United wamekuwa wakiukosa tangu kuondoka kwa Cristiano Ronaldo mwaka 2009.

Lucas anaweza kucheza kwa kwenye nafasi yoyote kati ya hizi tatu kwa mfumo wa 4-2-3-1 au kucheza upande wa pembeni kulia kwa mfumo wa 4-3-3.

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kumfananisha na Hulk au Pato, lakini wachambuzi wengi wa soka nchini Brazil wanasema mtu sahihi wa kumfananisha nae ni mbrazili mwenzie Gwiji Jairzinho.

Akiwa anafanana na mshindi wa kombe la dunia 1970 kwa mwili na staili ya kucheza, Lucas pia anavaa namba aliyokuwa akivaa Jairzinho (namba 7) kwenye timu ya taifa.

Sasa muangalie Lucas akiwa dimbani.

No comments:

Post a Comment