Search This Blog

Sunday, July 8, 2012

CHEKA AMKIMBIA JAPHET KASEBA ULINGONI TAMASHA LA MATUMAINI


Francis Cheka (mwenye T-sheti nyekundu) akitoka ulingoni baada ya kushindwa kupambana na Kaseba.
Katika hali ya kushangaza bondia Francis Cheka leo amemkimbia mpinzani wake Japhet Kaseba baada ya kugoma kupigana dakika kadhaa kabla ya pambano lao lilopangwa kufanyika leo uwanja wa taifa kwenye tamasha la matumaini. Cheka akizungumza na waandishi wa habari alitoa sababu ambazo kwa wengi zilionekana hazina mashiko - eti kwamba Kaseba sio saizi yake hivyo hawezi kupigana na mambo mengine yasiyo na maana. Kwa taarifa zaidi kuhus Cheka endelea kutembelea shaffihdauda.com
...Cheka na wapambe wake wakiukimbia ulingo.…

12 comments:

  1. aligundua dawa zake hazifanyi kazi ktk uwanja mkubwa kama huo akajua atapata aibu.

    ReplyDelete
  2. Alishachungulia kwenye tv asilia akaona hakuna uwezekano wa kushinda hilo pambano ndo maana amekimbia. Sababu alizotoa ni za kijinga sana. Huu aliofanya si uanamichezo. Shame on him

    ReplyDelete
  3. cheka hawezi pigana pambano halina ubingwa c ushaambiwa akipigana atapoteza taji lake? we vp shafii? we shabiki wa kaseba?
    acha zengwe

    ReplyDelete
    Replies
    1. kama alijua hayo alienda kufanya nn ulingoni?

      Delete
    2. Kama alijua alienda kufany nini? pia kwa nini alisaini mkataba wa kupigana? na huu mkataba aliasaini siku moja kabla y pambano lake alilopgana na mada maugo. Jamaa n mshirikina huwa akishaenda huko mtwara kwao ndo hufany maamuz apigane au la? Na hakuna pambano hata moja ambalo cheka amepigana bila y kwenda mtwara.Na wk tatu zilizopita cheka alikuwa huko, ali[porud tu ndo akasema kuwa hapigan.Baad y kutishiwa kupelekwa mahakaman ndo akakubar na mwishon nd hvyo hakucheza. Jamaa n mshrkina sana na kwa style yke hatofka popote.

      Delete
  4. SAFI SANA CHEKA KWA KUACHANA NA HILO PAMBANO.PAMBANO LILIKUWA NJE YA UTARATIBU WA KAWAIDA WA MCHEZO WA NGUMI.NA IKUMBUKWE CHEKA NI BINGWA KATIKA WA NGUMI KATIKA UZITO WAKE.SI SAWA MTU AKAJITOKEZA TU NA KUTAKA KUPIGANA NAE.NAWAPONGEZA SANA WALIOMSHAURI CHEKA KUACHANA NA HILO PAMBANO LISILO NA UTOFAUTI NA BONANZA.TUACHE KUMDHARAU CHEKA NI MTU MKUBWA SANA KWA MCHEZO WA NGUMI HAPA NCHINI.KAMA MASPONSA WANA NIA NZURI NA KIPAJI CHACHE WANAPASWA WAMTAFUTIE MAPAMBANO OFFICIAL YANAYOTAMBULIKA NA MASHIRIKISHO YA NGUMI DUNIANI BADALA YA KUMPELEKA KWENYE MABONANZA.
    BIP UP CHEKA NA WASHAURI WAKO.

    ReplyDelete
  5. hana lolote huyo cheka kama aliyajua hayo mapema nini kilimfanya akubali kupigana?kakosa ustararabu,,

    ReplyDelete
  6. NYIE WAWILI MLIOCHANGIA HAPO JUU INONEKANA MNA KIZUNGUZUNGU CHA ULEVI WA JANA. KAMA CHEKA ALIYAJUA HAYO KWANINI ASITANGAZE MAPEMA KUJITOA? ALIFUATA NINI HAPO ULINGONI? MSIONGEE PUMBA KAMA MMENUSISHWA MAVI MAKAVU.

    ReplyDelete
  7. Cheka amefanya maamuzi mazuri sana coz kupoteza ubingwa kwenye bonanza ni upuuzi lakini alipaswa akatae mapema watu wamepoteza muda wao kwenda mpaka pale kisha hakuna pambano afrika oyeeeeee!!

    ReplyDelete
  8. Anategemea uchawi jamaa alishambiwa leo hatoki thuz y amekataa kupigana

    ReplyDelete
  9. CHEKA NA TIMU YAKO MMEFANYA MAAMUZI MAZURI...LENGO LILIKUA KUHIMIZA WATU WAJE WACHANGIE WATOTO WA KIKE KUPATA MABWENI NA MMETIMIZA HILO WEWE PAMOJA NA KASEBA KWANI WATU WENGI WAMEINGIA KWA AJILI YENU NA MABINTI SASA WATAPATA MADAWATI.SUALA LA KUPAMBANA HILO NI LINGINE KWANI HATA FLOYD MAYWEATHER HUWEZI KUMPAMBANISHA KWENYE BONANZA AKAKUBALI.HII NI KWA MABONDIA BINGWA WOTE WALIO MAKINI.

    ReplyDelete
  10. Hakuna lolote anamwogopa na amezoea kumvizia sasa kakuta jembe limejiandaa. Akaona hapa kitanuka ndo akatoka nduki.

    ReplyDelete