Search This Blog

Saturday, June 16, 2012

MPO WAPI VIONGOZI MLIOKUWA MKIITAKA KAMPUNI YA LIGI KUU YA VODACOM?

Zile mbio za vilabu nchini kushinikiza kudai TFF ibadili mfumo mzima wa uendeshaji wa ligi kuu Tanzania bara ambayo imekua ikilalamikiwa na wadau wengi wa soka nchini ziliota mbawa baada ya shirikisho la soka kuteua kamati ya ligi ambayo kwa baadhi ya wajumbe wake ni viongozi wa vilabu waliokua kwa pamoja wakipinga suala la mfumo mzima wa Kamati hiyo.

Katika vikao vyote ambavyo vilabu vilikaa, kwa pamoja walikubaliana kwamba uendeshaji mzima wa ligi uwe katika mfumo wa kampuni na kama haitoshi Agenda namba moja (No.1) ilikuwa ni kupinga kuendeshwa ligi kwa kamati. Viongozi wa vilabu kumi na nne (14) yani AZAM, AFRICAN LYON, KAGERA SUGAR, RUVU, COASTAL UNION, SHOOTING, VILLA SQUAD, SIMBA, YANGA, POLISI DODOMA, MTIBWA, TOTO, OLJORO, MORO, JKT RUVU waliteua viongozi wa kusimamia mchakato wakiongozwa na Mwenyekiti Geofrey Nyange Kaburu (Simba) Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesiga Celestine (Makamu Mwenyekiti), wakati Katibu Mkuu wa kamati hiyo ni Meja Ruta      ( Ruvu Shooting) na wajumbe ni Iddi Godigodi (Villa Squad), Evodius Mtawala (Simba), Said Mohamed na Shani kutoka Azam FC.
Kwa nia ya kuliendeleza soka letu na pia ni mwanzo wa vilabu kuwa na sauti moja inapofika suala la maendeleo katika medani nzima ya soka.

Vilabu pia vilionyesha jinsi gani vina uchungu kwani ilfikia kipindi hata vilabu kutishia kugoma kucheza mzunguko wa pili wa ligi ya VODACOM 2011/2012 kama ile ajenda yao namba moja(No.1) haitofanyiwa kazi.

Umoja wa vilabu ulikuwa dissolved naweza kusema mara tu baada ya Rais wa shirikisho Leodgar Tenga kuteua kamati ya ligi kama ifuatavyo :- Wallace Karia ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF( Mwenyekiti), Said Mohamed kutoka Azam (Makamu Mwenyekiti), huku wajumbe ni Mwanasheria Damas Ndumbaro, Yahya Ahmed (Kagera Sugar), Meja Charles Mbuge (JKT Ruvu Stars), Steven Mnguto (Coastal Union), Kaburu (Simba), Seif Ahmed (Yanga), ACP Ahmed Msangi (Polisi Dar) na Henry Kabera (Majimaji). Hapa nampongeza sana Tenga kwani alijua udhaifu wa viongozi wetu wa soka na ilifikia kipindi alithubutu kuwaita wengine wadogo zangu huku akijisifu kuwa yeye ni MBA holder na kwa kweli alifanikiwa kwani viongozi ambao walikua wakipinga kamati katika agenda yao No.1 waliingia kwa moyo mmoja katika kamati ile yani (Nguruwe sili maini yake nakula)

Viongozi hao walikwenda kufanya kazi za kamati ambazo ni kuongeza vurugu katika soka kwani tumeshuhudia jinsi kamati hii ilivyokuwa ikitunishiana misuli na ile ya mzee wangu kamanda Alfred Tibaigana kwa maana sio tena kamati ya ligi na kuishia kufanya kazi za kamati ya sheria na kuleta vurugu kubwa sana mwishoni mwa msimu wa ligi.

Ni aibu kubwa kwani katika mambo ambayo tuliyapa kipaumbele yalikuwa ni Ligi daraja la kwanza suala zima la udhamini sasa angalia leo Fainali za ligi daraja la kwanza mkoa una invest fedha ili kupata fursa ya kuandaa fainali husika na hatimaye timu kutoka kituo mwenyeji kupanda kucheza kigi kuu Tanzania bara na hili tumelishuhudia miaka 4 mfululizo.

Ligi imekwisha viongozi wanahaha mara Zambia, Kenya, Uganda, Malawi, Rwanda na wamesahau kwamba mkataba wa Vodacom inabidi uangaliwe upya kwa vilabu kushirikishwa au kama wamekubali timu ndogo ziendelee kuambulia 5700/= gate collections Chamazi watuambie.

IDDI GODIGODI

No comments:

Post a Comment