Search This Blog

Monday, June 18, 2012

MAONI YA MDAU : MPIRA WETU UMEJAA SIASA NYINGI

Mimi kama mpenzi wa mpira na mtanzania nimeudhunishwa sana, kusikitishwa na kufadhaishwa kwa kitendo cha taifa starz kutolewa na msumbiji ktk michuano ya kombe la dunia.
Nna huzuni ingawa matokeo hayo niliyategemea kwa asilimia kubwa,
Mpira wetu umekuwa na siasa nyingi na falsafa yetu ya kujenga timu, kila mwaka na kila kocha anayekuja huwa ana kazi ya kujenga timu tu,.
Kuna maswali yaniniumiza kichwa sana, maswali hayo ni:-
1. Jan paulsen alikuja na kupewa mkataba wa miaka miwili, je ushawahi kuona wapi timu ikajengwa kwa miaka 2?
2. Kim paulsen ana mkataba wa mwaka mmoja, je atajengaje timu kwa mwaka mmoja? Au atafanya kila namna tu ili atufurahishe kwa huu mwaka mmoja aliopewa.
(ntaomba majibu kwa maswali hayo)
kama tungelikuwa na mipango ya muda mrefu toka alipokuja maximo mwaka 2006 ina mana huu ungekuwa ni mwaka wa 6 hvyo tungekuwa tumeshajenga timu nzuri na hapana shaka na sie tungekuwa ni washiriki wa AFCON mwakani, pamoja na WORLD CUP 2014.
MAPENDEKEZO YANGU NI:-
1.Kocha apewe mkataba wa miaka minne na awe na jukumu la kujenga timu haswa kwa kuwatumia U-20 na U-23.
2.Timu isishiriki kwa kipindi fulani mashindano yoyote kama ya AFCON au wORLD CUP na badala yake tujikite katika kuijenga timu na kuipa mechi nyingi za kirafiki zitakazochezwa ndani na nje ya nchi.
3.tutumie mashindano ya CECAFA kama njia mojawapo ya kuijenga timu yetu, haswa kwa kuwatumia hao vijana.
4.katika hiyo timu kuwe na wakongwe wasiozidi wanne ambao watakuwa na jukumu la kuwapa uzoefu vijana hao.

tukifanya hvyo tutakuwa tumejenga timu yetu badala ya kutumia vibaya rasilimali zetu huku tukijua fika kuwa hatufiki kokote zaidi ya kuwa wasindikizaji tu.
Ahsante kwa kunipa nafasi.
Huu ndio mtazamo wangu.
Naomba kutoa hoja.
IBRAHIM SHAWEJI
0717183929

2 comments:

  1. Umejitahidi kutoa maoni yako mazuri sana.Ongera sana kwa kuwa mzalendo. Lakini ndugu yangu timu haikomai kwa mazoezi peke yake. Timu bora ni ile yenye maandalizi mazuri kama ulivyosema pamoja uzoefu wa kutosha katika mashindano.Ili tuwe na timu bora ni lazima tushiriki mashindano mengi sana kwa kutumia hao vijana wetu wadogo.Mashindano yanamfanya mchezaji ajiamini zaidi kuliko mechi za kirafiki peke yake. So ni kweli kabisa lazima tuwaaandae vijana wa U17 na U20 kwa muda mrefu wakiwa na kocha mmoja then tushiriki kila mashindano yatakayokuja mbele yetu. Tusiogope kufungwa bila kufungwa hatuwezi kujirekebisha makosa yetu.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli ni idea nzuri lakini kujitoa atika mashindando siyo sahihi me nadhani ni vizuri kushiriki tu na kupata uzoefu,mechi za kirafiki haziwezi kuwa kipimo pekee kwa timu yetu na pia mashabiki angalau tumeanza kubadilika kimtazamo kuhusu timu yetu ya taifa na naamini njia bora n sahihini kuwa wavumilivu tu

    ReplyDelete