Search This Blog

Monday, June 18, 2012

KIFUKWE NA MANJI SI WADHAMINI HALALI WA YANGA!

Mwananchama wa Yanga bwana Abeid.A. Abeid ameibuka na kuwekea pingamizi uchaguzi wa klabu ya Yanga kwa kile anachodai katiba iliyotumiwa na wagombea si halali.
Bwana Abeid amabye aliwahi kuwa mweka hazina wa Yanga siku za nyuma pia amedai ndugu Yusuf Manji na ndugu Francis Kifukwe si wadhamini halali wa Yanga.

6 comments:

  1. WAPUUZI KAMA HAWA KINA ABEID WATAISHA LINI? WANATAKA KULETA MIGOGORO MINGINE. KAMA SI WADHAMINI HALALI MBONA MLIKUWA MNACHUKUWA PESA ZAO. ACHA NJAA YAKO WEWE. TAFUTA KAZI UFANYE TUACHIE YANGA YETU. NYINYI NDIO MNAFURAHI YANGA KUFUNGA TANO. MWANACHAMA MWANACHAMA, MWANACHAMA KITU GANI. NDIO MAANA MIMI NASEMA KILA SIKU HAYA MAMBO YA WANACHAMA YAFE TIMU ZIWE KAMPUNI TUBAKI MASHABIKI, WAKEREKETWA, WAFURUKUTWA TU. NDIO MAANA TIMU ZETU ZA SIMBA NA YANGA HAZIISHI MIGOGORO KWA WAPUUZI KAMA HAWA.

    ReplyDelete
  2. wanayanga tusikubali kurudi nyuma,hao kina Abeid wamefilisika.Yanga daima mbele nyuma mwiko.

    ReplyDelete
  3. wanayanga tusirudi nyuma

    ReplyDelete
  4. Mpuuzi kabisa apeleke njaa zake kama anajua kuna wazamini halali alikuwa wapi wakt timu inazuiwa Arusha atafute klabu yake atuachie yanga yetu huo upuuzi apeleke kwao kama ana hela angesadia pale yanga walipokwama mwanza hawa ndo vijino pembe

    ReplyDelete
  5. Wadhamini wanaoongelewa hapa sio wa kutoa hela kwa maana ya sponsors, wadhamini anaongelea huyu mtoa pingamizi ni waangalizi, wasimamizi kwa maana ya trustees, mfano utasikia wanasema bodi ya wadhamini ya Yanga hii sio bodi ya watoa hela ni bodi ya wasimamizi, kwa hiyo mtoa maoni wa kwanza na wa nne msimlaumu jamaa kwamba alikuwa anachukua hela kwa hao wadhamini, kama walikuwa wanatoa hela kama wadhamini (trustees)basi hiyo walipenda wenyewe lakini hawakulazimika kutoa hela wao kazi yao ilikuwa ni kusimamia, kuangalia mali za Yanga.

    Nilitaka tu nifafanue ili siku nyingine mtoa maoni mkiwa mnaelewa mnachoongea otherwise hayo ni mambo yenu watu wa Yanga sisi wa mtaa wa pili hayatuhusu.

    ReplyDelete
  6. Yale yote yaliyokwisha tokea mpaka kumtoa Nchunga yalikuwa ni Trailer, Movie inaanza sasa.Vituko havitakuja kuisha ndani ya hivi vilabu, haya sasa wakati wao wanashikana mashati kagame nayo inajongea wao kama mabingwa watetezi sijui wanategemea nini, kocha hajulikani ni nani,Maximo anasema hili yanga nao wanasema lile.
    Yetu macho na masikio.Ila Manji kama kweli anaupenda mpira akae pembeni aanzishe timu yake, mimi nina unakika kwa hela alizonazo akianzisha timu ndani ya miaka miwili inakuwa kama Azam.Ama kama vipi akanunue timu iliyoko daraja la kwanza aanzie hapo anaweka infrastructure za uhakika anaachana na mizengwe naamini angeheshimika zaidi kuliko kujiingiza mahala penye matatizo ambayo mwisho wa siku yatamvunjia heshima tu.Hakatazwi kuwa na timu yake nabado akaisaidia yanga kama kweli anamapenzi nayo, ila kwa kuwa na timu yake angeonyesha njia kama walivyoonyesha Azam.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete