Search This Blog
Sunday, June 3, 2012
CELEBS BATTLE: DIAMOND VS BOB JUNIOR
DIAMOND PLATNUMZ
1: Who's the best artist between you and Bob Junior?
Everbody knows that Diamond ni hatari kuanzia kimashairi, kuimba, mpaka kwenye performance, that's why kila siku napiga show nje kuanzia Italy, Sweden, Holland, na Greece.Mkata viuno cant touch this milele.
2: Unadhani Bob Junior asingekuwa mwanamuziki angekuwa nani?
Haihitaji kuongea sana kuhusu hili, kutokana na kujua kukatika kama Fifi Moto, basi ningemuajiri kama mcheza shoo wangu.
3: Nani anamiliki mtoto mkali?
My galfriend is best thing that Bob Junior will never have, hivyo sihitaji hata kusema zaidi nisije nikakufuru bure.
4: Which one is the best "Wasafi" or "Sharobaro"?
Wasafi ndio kila kitu, tunajua kupendeza, kutafuta mkwanja na ndio maana tuna maendeleo.What's hell is Sharobaro?
5: Kwa mitupio nani anamuongoza mwenzie?
We mimi noma, wajanja wa town wanakoma na pamba zangu, Sharobaro atabaki kuwa Junior kwenye suala hili and i'll alwayz be his senior.
6: Out of 10, unampa ngapi Bob Junior kama mwanamuziki?
Nafikiri tatu zitamtosha kabisa.
7: Imagine upo ulingoni na Bob Junior, Shabaro angedumu kwa round ngapi?
Round ya kwanza hamalizi, nitampiga kwa KO kali hadi madokta wa hospitali waombe PF3 ya IGP Mwema.
8: Nafasi ya kumshauri Bob Junior hii hapa, unamshauri nini?
Aongeze juhudi katika uproduyza, na akubaliane na ukweli muziki wa Diamond ni platnum, hivyo asijaribu kushindana nao.
BOB JUNIOR
1: Nani msanii mkali kati yako wewe na Diamond?
Mimi ni zaidi ya msanii, najua kuimba, kucheza, napigwa karibia vyombo vyote vya muziki.Mimi ni mwanamuziki niliyekamilika Diamond yupo nyuma sana.
2:Diamond angekuwa msanii, kazi gani nyingine ingemfaa?
Udalali ungemfaa sana, kwani alishawahi kunikodishia watu Coaster nzima waje kwenye show kunizomea Billz.
3: Between you two nani ana demu mkali?
Demu wangu is the finest chick in town, kuanzia reception, figure, mpaka maadili sidhani kama demu wa Diamond ana sifa hizi.
4: Nani anatisha kati ya "Wasafi" na "Masharobaro"?
Masharobaro we are best in town kwa sasa, tumethibitisha kwa mambo mengi ikiwemo kumtoa Diamond kimuziki.Masharobaro a.k.a Mashombeshombe ni hatari.
5:Kwa kunyuka pamba nani anamfunika mwenzie?
Mimi ni raisi wa masharobaro, wasafi na watanashati duniani, Do you think Diamond anaweza kugusa huu moto? aaah you cant be serious¡¡¡¡¡¡¡¡¡¡.
6: How would you rate Diamond out of 10/10?
Nawaachia fans wamchagulie ngapi apewe chini ya namba 4.
7: In the ring wewe na Diamond, nani angeibuka mshindi?
Sekunde 10 za raundi ya kwanza pambano limeisha, maana nitapiga upper cut chini ya kidevu, mtoto wa Tandale chaliiiii.
8: Unapewa nafasi ya kumshauri Diamond, unamwambia nini?
Aende shule akajifunze muziki, ili aweze japo kufikia robo ya level yangu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Diamond the best.mkata miuno uupate moto huu ww,chezea wasafi ww.
ReplyDeleteEbanaaa hii kali wamehojiwa wapi na nanii hii?na watashindishwa lini
ReplyDeleteally albusaidy
Pasipo kuwa na upendeleo wowote kwanza kabisa kwa kusoma tu majibu yao ningewapa alama zifuatazo.Diamond 8/10 na Bob Junior 4/10, kwanini Mwanaume unapoanza kujisifia kwamba wewe ni shombe shombe huo ni upuuzi wa watoto wa kike shombeshombe then what.....Lingine unaposhindwa jambo usisukumie sababu kwampinzani wako yeye Junior anasema alizomewa jukwaani na kisa eti Diamond alimkodishia watu wakamzomee hakuna kitu aongeze bidii asitafute sababu anafanya shoo chini ya kiwango ndio maana anazomewa.
ReplyDeleteUkali wa Diamond hauna utata pamoja na madhaifu yake yote ila Bob Junior kwa Diamond ana kaa round ya kwanza.Bob Junior ana hit single 2 ataimba nini baada ya hizo single 2.
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni tu Diamond, he is in the next level when compared to Bob junior.
Mdau
Mike
inafurahisha na kusikitisha zaidi,kufa si mpaka roho itoke lakini unaweza ukawa umekufa na bado unatembea.
ReplyDeletediamond ni noma
ReplyDeleteBob is the best. Music sio kuimba na kuwa na scandals za wanawake mtaani. The Guy anaimba, tena bonge moja la vocalist, anaandaa beats, nice dances, Good look..... Bob Junior kaza buti brah achana na huyo dogo, umemlea mwenyewe huyo
ReplyDeleteAlee ye mzazi kubali msikubali acheni mtt wa kimanyema atambe bwana ashataabika kitambo sana kipindi alivyojaribu kuflow na hip hop.... jamaa studio ndo imemtoa so haijalishi angeenda hata kwa AM records kwa maneck angetoka!!!!! Tuacheni ushabiki wa kilimbukeni Bob junior bado mdogo sana kwa Diamond platnumz.... Binafsi sijawahi ona show ya Diamond mbaya
ReplyDeleteUshauri: Bob junior umesoma music mpka instrumental lkn u dont hav wat it takes kufika kwa PLATNUMZ level so kaza BUTI alafu acha maringo bwna
Mimi kwa maoni yangu naona watu tunatoa comments kiushabiki zaidi kuliko hali halisi. Kwa maoni yangu wote ni wanamuziki wazuri na ndio maana ni rivals kwani siku zote mafahari wawili hawawezi kukaa kwenye zizi moja.
ReplyDeleteKati ya hawa jamaa wawili kila mtu ana kipaji chake zaidi kumzidi mwenzake. Nafikiri kama tunazungumzia kuimba na kutoa hits zinazotamba Diamond yuko kwenye form kwa sasa lakini kama tunaangalia muziki kwa ujumla kwakweli mtu kama BOB JUNIOR huwezi kumkejeli hata kidogo na haswa DIAMOND mwenyewe. Jamaa yuko juu na sidhani kama wameshatokea "Maprodyuza" wa Bongo Fleva wangapi nchini ambao pia wameweza kuwateka watu kwa kuimba muziki wao wenyewe hadi kukubalika na watu. Unajua hiki ndio tunapaswa tujifunze sana sisi WATANZANIA hasa wasanii na wanamichezo kwa ujumla, yaani kuwa "Professional" katika kila kitu. Nilitegemea DIAMOND pamoja na uhasama wote waliokuwa nao na BOB JUNIOR angejaribu hata kumpa respect inayostahili ambayo ni kumtoa kwenye soko la muziki hiki ndicho alichotakiwa kufanya pamoja na kejeli nyingine zote alizotoa.
Kwa ujumla DIAMOND tunamkubali katika eneo lake (Yaani kuimba na kuperform) lakini vile vile lazima tukubali kwamba huyu BOB JUNIOR ni exceptional maana ameonyesha ana kipaji cha hali ya juu kwa kuwa na uwezo wa kujua vitu vingi sana katika muziki kuliko DIAMOND