Search This Blog

Wednesday, May 30, 2012

ZIARA YANGU KWENYE UWANJA WA KISASA ZAIDI BARANI ULAYA - ALLIANZ ARENA

Siku moja kabla sijaondoka jijini Munich, nilipata nafasi ya kuungana na baadhi watu wakiwemo waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni kuweza kutembelea uwanja wa kisasa zaidi duniani Allianz Arena unaotumia na klabu ya Bayern Munich na TSV 1860 Munchen.

Muda wa saa saba za mchana tukawa tumefika kaskazini mwa jiji la Munich ulipo uwanja huo, ambao ulianza kujengwa mwaka 2002 na kukamilika miaka miwili baadae kabla ya kufunguliwa mwaka May 30, 2005.

Gharama za utengenezaji wa dimba hili zinakadiriwa kufikia €340million, huku jiji la Munich likitumia kiasi cha €210 million kwa ajili ya kuliendeleza eneo ulipo uwanja huko - pamoja na matengenzo ya miundombinu.

Uwanja huu kwa sasa unasimamiwa na Allianz Arena Munchen Stadion GmbH, ambao walinunua haki za jina la uwanja kwa miaka 30 - lakini jina la Allianz huondolewa kwenye mechi ambazo zinaandaliwa na UEFA na FIFA. Lakini uwanja huo ulikuwa unamilikiwa kwa share sawa na klabu mbili zinazoutumia uwanja huo kama dimba la nyumbani.
Mwaka 2006 FC Bayern Munich walinunua asilimia 50 ya share za TSV 1860 Munchen kwa Euro 11 million - hivyo kwa maana hiyo uwanja huo kwa sasa unamilikiwa kwa asilimia 100 na FC Bayern Munich.

Uwanja huu unaingiza watu 66,000 mpaka 66,901 kutegemeana na mechi. Ndio uwanja wa kwanza duniani ambao unadilika rangi kutokana na timu zinazocheza.

Goli la kwanza kabisa kwenye za ushindani lilifungwa na kiungo Owen Hargreaves wa FC Bayern Munich katika mechi ya ufunguzi wa msimu wa Bundesliga 2005-06 dhidi ya Borussia Monchengladbach. 



1 comment:

  1. Kaka shaffih Dauda kwanza nimefurahi ur back to sport xtra baada ya tour yako ya Europe. Uwanja wa Allianz Arena na uwanja wa Wembly wa Uingereza ni upi wa kisasa zaidi mkuu? ulipozungumza suala la uwanja umenikumbusha suala la SIMBA ARENA hivi lile suala la simba kujenga uwanja wao liliishia wapi kuna wakati tuliona jamaa wametoka uturuki na ramani jinsi uwanja utakavyo kuwa ila ghafla naona kimya ama ilikuwa ni siasa kama kawaida ya wabongo hawa jamaa mbona suala la uwanja linawezekana ila hawataki kabisa kuwa serious na suala la kujenga kiwanja, mimi huwa sielewi nini tatizo hasa la simba ama yanga.
    Shaffih ile makala ya yule beki wa yanga mbona umeipotezea tena mkuu
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete