Zikiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya timu ya Taifa ya Tanzania kusafiri kwenda kuwavaa Ivory Coast - taarifa rasmi kutoka kambi ya timu hiyo zinasema kwamba mshambuliaji Tom Ulimwengu hatosafiri na timu hiyo.
Ulimwengu, mshambuliaji chipukizi wa timu ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ameshindwa kupona maumivu ya kifundo cha mguu aliyopata akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Mbali na Ulimwengu Taifa Stars pia itakuwa bila ya kiungo wa kutumainiwa wa Yanga Nurdin Bakari ambaye pia ameshindwa kupona maumivu ya nyama za paja yaliyokuwa yanamkabili. Ulimwengu na Nurdin wote walikosa mchezo wa kirafiki ulioisha kwa sare ya bila kufungana dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi uliochezwa Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita.
Ofisa wa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) alisema jana kuwa amepata taarifa kutoka kwa daktari wa timu ya taifa Mwanandi Mwankemwa kuwa wachezaji hao hawatasafiri na kikosi cha timu hiyo kinachotarajiwa kuondoka keshokutwa alfajiri kwa ndege ya Shirika la Kenya kuelekea Ivory Coast. Hata hivyo kocha wa Stars Kim Poulsen amesema hatoita wachezaji wengine badala yake waliopo watajaza nafasi za nyota hao.
Katika mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya Malawi Kim alimchezesha nyota wa TP Mazembe Mbwana Samatta na kiungo mchezeshaji wa Simba Haruna Moshi ‘Boban’ kwenye nafasi ya ushambuliaji, huku Shaabani Nditi wa Mtibwa Sugar, Mwinyi Kazimoto wa Simba na Franka Domayo wakicheza kwenye nafasi ya kiungo.
Katika mechi hiyo kocha Kim alifanya badiliko moja kwa kumpumzisha beki wa kushoto wa Azam Waziri Salim na nafasi yake kuchukuliwa na Amiri Maftaha aliyeonekana kidogo kuubadili mchezo huo.
Hata hivyo Kim baada ya mechi hiyo alikiri kuwa anaweza kukifanyia mabadiliko kikosi cha timu hiyo kilichocheza dhidi ya Malawi lakini alisema hilo litategemea na namna atakavyoona wachezaji wake wanavyocheza mazoezini katika siku hizi zilizosalia kuelekea mchezo huo.

Habari kaka,
ReplyDeleteAhsante sana kwa habari za uhakika katika muda muafaka unazotupatia.
Katika habari hii, mbali na kuvutika na habari yenyewe lakini pia nimevutika na kujiuliza maswali mengi na hiyo kaptula (bukta) ya Ulimwengu uliyoongezewa namba 3 kwa marker pen. Nimejiuliza maswali kama, jee namba ilibanduka? au hakukuwa na bukta namba 23 au ............
Get well soon guys
Kila la heri Stars,
de bebeto.