Search This Blog

Saturday, May 26, 2012

TAIFA STARS YATOKA SARE NA MALAWI - YAJIWINDA KUWAKABILI AKINA DROGBA

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania - Taifa Stars leo imetoka sare tasa dhidi ya Msumbiji kwenye mchezo kirafiki kuelekea kwenye mechi ya kugombea nafasi ya kucheza KWENYE KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014 dhidi ya Ivory Coast.
Mchezaji wa timu ya taifa Taifa Stars Mbwana Samata ambaye anacheza mpira wa kulipwa katika timu ya TP Mazembe nchini DRC Congo akijaribu kumtoka beki wa malawi Foster Namwela wakati timu hizo zikimenyana kwenye uwanja wa Taifa jioni hii
 Wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars wakiingia uwanjani jioni hii kwa ajili ya kupasha mwili kabla ya mpambano wake wa kirafiki na timu ya taifa ya Malawi The Flames
 Wachezaji wa timu ya Malawi wakipasha mwili kabla ya kuingia uwanjani kukwaana na Taifa Stars jioni hii kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Taifa Stars wakijifua kabla ya mpambano huo jioni hii.

2 comments:

  1. Kila Siku draw ndio Ushindi wetu! Kweli hivi nchi soka liko chini sana!

    ReplyDelete
  2. Najiuliza hawa msumbiji tuna mechi ya marudiano ya ushindani leo tunacheza nao ya kirafiki,HIVI TUPO MAKINI KWELI?!

    ReplyDelete