Search This Blog

Saturday, May 5, 2012

STEWART DOWNING: NAMCHUKIA DI MATTEO NA LEO NITALIPIZA KISASI DHIDI YAKE.

Roberto Di Matteo akifunga goli dhidi ya Middlesbrough.
Roberto Di Matteo  tayari alishamuumiza moyo Stewart Downing - lakini sasa winga huyo wa Liverpool yupo tayari kulipiza kisasi leo hii.

Mwaka 1997, Downing akiwa na miaka 12, akiwa mmoja ya wanafunzi wa shule ya soka ya Middlesbrough alienda Wembley akiwa na matumaini kibao kwamba klabu yake ya nyumbani itatwaa taji la FA Cup.

Lakini ya sekunde 42 Chelsea walikuwa mbele shukrani kwa goli la mita 25 la Roberto Di Matteo.

Liverpool star Downing alisema: “Wote tunakumbuka goli la mapema la Di Matteo likiingia nyavuni. Nimemchukia tangu wakati huo!Majina niliyomuita siwezi hata kuyarudia, lakini alikuwa mchezaji mzuri na anafanya vizuri kama manager akiwa na Chelsea. Leo nataka ayasikie machungu ambayo yameniandama kwa zaidi ya miaka 15."

No comments:

Post a Comment