Search This Blog

Wednesday, May 23, 2012

SIMBA KUIPA FAMILIA YA MAFISANGO FEDHA NYINGI - KWA MARA YA KWANZA - KUWEKA HISTORIA YA KUTEMBEZA KOMBE MITAANI

 
Baada ya kutoka taarifa za kwamba wiki hi klabu ya Simba itafanya sherehe za kushangilia ushindi wa kombe la VPL baadhi ya mashabiki tofauti wamekuwa wakitoa maoni hasi juu ya uamuzi wa klabu hiyo kufanya hivyo wakati ikiwa imefiwa na mchezaji wao Patrick Mafisango wiki iliyopia tu. Hivyo leo kupitia mtandao wa Facebook msemaji wa simba alijibu maoni haoa kama ifuatavyo.

Ezekiel Kamwaga - Msemaji wa Simba
Nimesoma sana maoni ya watu kuhusu show ya Simba DarLive.... Nakubaliana na karibu wote waliotoa haki yao. Kwanza mimi ni nani au Simba ni nani hadi isikubaliane na maoni ya watu? Lakini ningependa kusema machache kuhusu maoni ya watu.... Mosi, watu wa mpira wanajua kwamba kuna kitu kinaitwa logical reason na footballing reasons. Kwamba kuna mahali inabidi soka ifanywe soka na logic ibaki kuwa logic. Ndiyo maana kuna msemo kwamba Common Sense Is Not Always Common. Nitafafanua....Alipokufa uwanjani Marc Vivien Foe miaka kumi iliyopita, pambano liliendelea kama kawaida.... It was not logical reason, it was footballing reason.... Mara baada ya kifo cha mchezaji Antonio Puerta wa Celta Vigo mwaka 2007, siku tatu baadaye Celta ilicheza na AC Milan, na ikatangazwa kuwa ni kwa heshima ya Puerta, hata kama kuna wachezajiu walishindwa kucheza.... Footballing reason... Maisha si mali ya binadamu.... Hebu tuseme hivi, Kama Simba itasubiri hadi arobaini ya Mafisango ipite ndipo ifanye sherehe na kwa bahati tukapata msiba mwingine siku ya 35, je, itabidi tuahirishe tena kwa siku nyingine 40? Au Taifa likapata tukio ambalo litasababisha tuingie kwenye maombolezo, au Mungu apishilie mbali, itokee kitu kinaitwa Force Majeure kwa lugha ya kisheria (an act of God) kama vile tsunami au tetemeko la ardhi, tutafanyaje? Tutaahirisha tena? Kwa wanaomjua vema Mafisango, kama angeulizwa huko aliko (Mungu amweke mahali pema peponi) yeye angekuwa wa kwanza kuturuhusu tufanye sherehe yetu ya ubingwa.

Nimebaini kwamba wako watu ambao wanataka kuonyesha kwamba Simba haina huruma au haijaguswa kabisa na msiba wa Mafisango kuliko wao. Baadhi yetu tumeishi na Mafisango, tumelala naye, tumefanya naye mazoezi na tunamjua kuliko baadhi ya watu ambao wametoa comments... Sasa najiuliza, hivi mwenye uchungu na Mafisango ni nani haswa? Yule ambaye aliamka saa kumi alfajiri na kwenda Muhimbili kuhakikisha amehifadhiwa vizuri na kumuandalia msiba na mazishi ya kitaifa au yule ambaye analalamika tu kila kukicha? Simba ina uchungu sana na Mafisango lakini It is a football club na lazima maamuzi yake yana base kwenye football na si common sense au mila za kiafrika.

Kufanya sherehe kwenye mazingira haya ni kumuenzi pia Mafisango. Timu inachukuaje ubingwa na kukaa tu kana kwamba hakuna kilichofanyika? Tusisahau kwamba kinachofanyika mwaka huu ni kitu kipya... Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 75 ya Simba kufanyika Bus Tour.

Hii ni kama Pilot Project.... We can only get better....Mwakani, tutachukua on board yale mapungufu ya mwaka huu na kufanya kitu kizuri zaidi.... Lakini, mnaupondaje uongozi kwa kujaribu kufanya kitu kizuri... Mbona mwaka juzi hakuna miongoni mwenu aliyetoa wazo la Bus Tour? Kwanini Watanzania tumekuwa na tabia ya kutaka kuponda tu kila kitu badala ya kutoa maoni ya kurekebisha ili twende vizuri.

Kuna mtu hapa anaitwa Mohamed Mashango, naona yeye anajua kuponda tu....Anafikia hatua ya kulinganisha Simba na timu ya mtaani kwake ya Kitintale.... Haya ni matusi kwa Simba, lakini ndiyo aina ya washabiki wa Simba tulionao !

Simba haijui kufanya sherehe? Nani anafanyaga Simba Day kila mwaka? Ni klabu gani nyingine ina utaratibu wa kufanya kitu kama Simba Day katika ukanda huu wa Afrika Mashariki? Kuna klabu gani imewahi kufanya party ya kiwango cha juu hapa Tanzania kama wakati tunazindua Simba TV? Mashango anapata wapi ujasiri wa kuilinganisha Simba na Kitintale? Glorie namuonaga uwanjani na hata mazoezini wakati mwingine lakini sijui kama huyu Mashango anakuja hata mpirani.... Au anaangaliaga ya Kitintale?

Niwafahamishe pia kwamba mpango wa kusaidia familia ya Mafisango upo...Iwe kwa kuandaa mechi au namna nyingine yeyote.... Muhimu zaidi ni kwamba Simba itafiwa tena na tena. Na imewahi kufiwa huko nyuma pia.... Cha msingi ni kwa klabu kuweka utaratibu wa kusaidia familia za wachezaji wake wote katika siku zijazo... Hili ndilo klabu inalolipanga kwa sasa.... Lakini naomba niwaambie kitu kimoja, familia ya Mafisango itapewa fedha nyingi na Simba.... Kiasi ambacho hakuna klabu yoyote ya Tanzania au Afrika Mashariki imewahi kukitoa kwa familia ya mchezaji aliyefariki.

You can take my word on that..... Niseme mwishoni kwamba inawezekana ukumbi wa DarLive si mzuri, yes, we can take that on board.... Inawezekana washabiki hawajapenda kuweka viingilio, we can take that on board..... Pengine watu wangependa sherehe hizo ziandane na utoaji tuzo kwa wachezaji, hilo pia ni wazo zuri. Ninalichukua.

Ningetaraji michango ya namna hiyo kwa Wana Simba.... Si kusema hatujui kupanga sherehe, hatuna uchungu na Mafisango au tuna tamaa ya fedha.....

Ningeomba tushiriki kwenye sherehe za mwaka huu na tujiandae kwa sherehe nzuri zaidi, za kiwango zaidi na zenye ubora zaidi msimu ujao.... Hiyo ndiyo Simba.

7 comments:

  1. Siamini kama ni kauli za kiongozi,hakika hajazungumza na kujibu hoja za wadau,amefanya personal attack na sio hoja attack,leo chelsea hawashindani lini na wapi na nani amefanya sherehe kubwa wanaangalia nani kachukua UEFA mara nyingi na wao wafiikie,kiongozi ana uliza nani kafanya sherehe kubwa!anatakiwa kusema why simba inafanya sherehe wkt bado wanamajonzi,je mafisango ataenziwa vp,lol

    ReplyDelete
  2. huyo ndiye ezekiel kamwaga,mropokaji wa timu ya simba

    ReplyDelete
  3. Watu wasichanganye mambo kwani kufanya sherehe ni moja ya kumuenzi Mafisango hoja kwamba ni wakati wa majonzi haina mashiko kwani kwa mjibu wa ratiba ya sherehe hizo viongozi, wachezaji na mashabiki watapata wasaa wa kumkumbuka shujaa wetu mafisango na kuuenzi mchango wake hivo ni vema wanasimba tukajitokeza kwa wingi Dar Live.

    ReplyDelete
  4. sherehe inaweza kufanyika kama kawaida ya mafisango yameshapita ndugu,, muhimu kwasasa ni namna ya kuisaidia familia yake basiiiii! wiki moja nitosha kabisaa kwa club kuomboleza msimba hii si familia ya mtu mpaka arobaini ifanyike,, kwanza what's arobaini anyway? acheni uswahili kwenye mpira,, nataka kuliona kombe kwa bus la wazi na hao wapingaji ni wazee wa mangumi tu!

    ReplyDelete
  5. jaman mim sio shabiki wa mambo ya footbl wala sijui sana haya mambo ya mpira,ila wabongo nawajua sana.how cm hapa linaonglewa swala la shrhe in cnctn na msba mtu anahoj why smba hawafkrii kuchkua vkombe,thts nonsens instead!mst of sis watz ha2shuhulsh mind ze2 ktk kusolv matatzo 'wht shld b done' rather tuko vzur sana ktk kupoint fingers,kufanya sherhe kpnd cha majonz ts nt a prblm only tht huyo kiongoz angeeleza kua hyo shrh itarecogniz vp hi moment ya majonz apart frm ile silent mmnt,may b mnge2mia jez yake au jina lake-any thng kuimark hyo cku muhmu kwenu na memories of the late mafisango.

    ReplyDelete
  6. Ezekiel ametoa majibu mazuri na ufafanuzi mzuri.Wewe unayepinga andika namba yako ya uanachama wa Simba or hit the highway.Njoo na na fikra mbadala sio kuponda tu.

    ReplyDelete
  7. mashabiki wengine sijui wanaupeowakiasi gani, kwani nilazimehuende? kama unaona haina maana,kaanyumbani kwako,wanaofahamuumuhimu wake wataenda. Ezekiel kamwaga yupo very right. wabongo wanajua kuropokatu,mwambie aje na mbinu/mpango mbadala hana. wengine wameshazoea kuiga tu, eti chelsea,au clab za ulaya hawajawahi kufanya, jamani tusizoee kucopy na kupaste. kama wazo ni jipya na linatija tulisaport na sio kuangalia kamalimesha fanyika paala pengine.

    ReplyDelete