Wakati Andres Iniesta na Xavi walipokuwa busy wakishinda Euro 2008, Alex Oxlade-Chamberlain alikuwa hana uhakika kwamba ataweza kucheza soka pale Southampton, achana kabisa na kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya England katika michuano ya EURO.
Lakini kuingizwa kwa mchezaji huyu kwenye kikosi cha Roy Hodgson kwa ajili ya Euro 2012, kunamfanya awe na deni kubwa kwa viungo wa Kihispania kwa kile walichokifanya mwaka ule.
Wakati huo, Oxlade-Chamberlain hakuwa hata haonekani kama ataweza kupewa mkataba wa kiuwanafunzi na Southampton kwa sababu alikuwa na umbo dogo sana. Mwaka mmoja baadae, alipofikisha miaka 15, alianza kutafakari nini atafanya huko mbele kama sio mchezaji wa soka.
Lakini miaka minne tangu Euro 2008, Spain wametawala soka la dunia, na wachezaji kama David Silva mwenye kimo cha 5ft 8in, David Villa - 5ft 7in, na Pedro mwenye urefu wa 5ft sawa na roho ya timu hiyo Xavi na Iniesta ambao wote nao wana urefu wa futi 5 - lakini wameiongoza timu yao ya tifa pamoja na klabu yao Barcelona kushinda makombe mawili ya ulaya, makombe mawili ya dunia ya nazi ya vilabu, na makombe matatu ya La Liga.

"Kwa mfano Iniesta aende kwenye kugombea mpira na kiungo mrefu wa kati mwenye manguvu, naamini kwenye raundi nane kati ya 10 atapoteza. Lakini Iniesta ana akili kuliko, anatumia touch yake ya kwanza kumpita mchezaji pinzani na kukaa mbele, hivyo mpinzani wake itabidi amchezee faulo au amuache aende mbele baada ya kupitwa.
"Inabidi ucheze aina hiyo ya soka kutokana na jinsi ulivyo mwenyewe na nafikiri hilo linakuja naturally. Ukijifunza kila siku, haijalishi una nguvu kiasi gani, inabidi ucheze kwa mtindo aina ya Iniesta.
"Ni mafundisho ya soka kwa yoyote, jaribu tu kuwaangalia Barcelona wanavyocheza. Namuangalia Lionel Messi, Iniesta na hata Cesc Fabregas. Siku zote napata vingi vya kujifunza kutoka wengine."
Mchezaji mwenzie wa Arsenal Aaron Ramsey anaamini kabisa atajifunza zaidi kwenye Euro 2012, akisema: "Alex amekuwa na msimu mzuri. Ni mdogo, anafurahisha kumuangalia, kwa hakika kabisa ana wakati mzuri sana huko mbele na nilifurahi sana alipoitwa.
"Kwa hakika kabisa amekuwa na anaweza kucheza kwenye hatua ya kimataifa."
Oxlade-Chamberlain alianza atleast kupata kimo alipofikisha miaka 16, wakati Southampton walipomuingiza kwenye kikosi cha timu ya watoto. Na hapo ndipo alipoanza kuondoa uoga kidogo kwenye kupambana na wachezaji wenye miili mikubwa.
Na katika kuonyesha kwamba ameanza kufaulu mafunzo aliyokuwa akiyapata kwa kuwaangalia akina Iniesta, aliweza kupambana na kumsumbua sana Mark van Bommel kwenye mechi ya Champions League dhidi ya AC Milan mwezi wa 3 mwaka huu - wakati kinda huyo alipocheza nafasi ya kiungo wa kati huku akipambana na mholanzi huyo - kwa hakika alionyesha kweli anaweza kupambbana vita yoyote na nguvu.
Siku zote amekuwa akipewa sapoti ya nguvu, na baba yake Mark ambaye aliichezea England kwenye miaka ya 80.
Mark alimwambia mwanae asiwe na wasiwasi kuhusu kutokuwa na na kimo kirefu, na badala yake aweke umakini katika kujifunza kuwa na ufundi na matokeo yake Oxlade Chamberlain ameendelea na kuwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa soka.
"Kama wewe ni mchezaji mwenye umbo dogo, inabidi uzoee kucheza na ubongo wako zaidi na kujifunza mbinu tofauti,: anasema Alex. "Na kama ukiweza kufanya hivyo, basi hilo litakuongezea uwezo zaidi utakapokuwa mkubwa."
Ikiwa Oxlade-Chamberlain atafanikiwa kuichezea England huko Ukraine, sio wazazi wake wala kaka yake, Christian, watakuwa pale kuangalia hilo.
Baba yake alisema wiki iliyopita kwamba uoga wa ubaguzi wa rangi umeizuia familia hiyo kwenda nchini humo.
Alex na baba yake George Eastham senior na junior, Brian na Nigel Clough, na Frank Lampard senior na junior ni muunganiko wa mababa na watoto zao ambao wote kwa pamoja wameiwakilisha timu yao ya taifa.
"Soka siku zote imekuwa sehemu ya maisha yangu, baba yangu alicheza," anasema Chamberlain. "Unapomuona baba yako anacheza na wewe utamani ujaribu na mie nilijaribu na nikapenda. Baba yangu hakuwahi kunilazimisha kucheza.
"Nilikuwa nafurahia kucheza na baba yangu alinisaidia. Alitumia muda mwingi kunifundisha, kunipeleka viwanjani na kunionyesha vitu tofauti pamoja na kuniongezea vitu kwenye mchezo wangu kiufundi. Siku zote alinifanya niupende zaidi mchezo huu."
Mark - baba wa Oxlade bado anafanya kazi nzuri katika kumuendeleza mwanae Chamberlain na soka lake kwa kukaa kuangalia michezo iliyopita kwenye DVD.
"Mimi na baba yangu huwa tunakaa pamoja sitting room na kuangalia michezo iliyopita kwenye DVD, tunafurahia sana kuangalia mpira, napenda kuangalia mechi nilizocheza na kujifunza zaidi kwa kuangalia kitu gani nafanya vizuri nikoreshe na wapi nakosea ili nisahihishe. Baba huwa ananiambia vitu tofauti na kunisahihisha ninapokosea. Tunaongea na kusikilizana na mwishoe nazidi kujifunza zaidi." - Alex
No comments:
Post a Comment