Search This Blog

Wednesday, May 23, 2012

NAMNA FC BAYERN MUNICH WANAVYOTENGENEZA FEDHA KUPITIA BRAND YAO - SIMBA, YANGA, AZAM JIFUNZENI


Kama nilivyoripoti jana kwamba nilifanikiwa kupata nafasi ya kufanya ziara kwenye makao makuu ya klabu ya Bayern Munich. Pamoja na kufanikiwa kutembelea sehemu mbalimbali zilizo ndani ya jengo la makao makuu ya timu hiyo, ikiwemo uwanja wa mazoezi, sehemu ya kuifadhia makombe waliyotwaa pamoja na kutembelea kwenye duka kubwa ambalo linauza vifaa tofauti vinavyotengenezwa kwa kutumia brand ya Bayern Munich.


Pamoja na kujifunza vitu vingi kwenye ziara yangu ya jana, lakini kubwa zaidi ni jinsi FC Bayern Munich inavyoweza kujiendesha kibiashara na kuweza kutengeneza pesa nyingi kupitia bidhaa tofauti wanazotengeneza na kuziuza.


FC Bayern kupitia brand yao wanatengeneza aina zote za mavazi kuanzia Kofia, mashati, soksi, fulana, skafu, vitambaa vya jasho, suruali za aina zote, viatu vya aina zote kuanzia vya michezo mpaka vya kawaida yaani kifupi kila aina mavazi wanatengeneza. Pia wanatengeneza vitu kama vifaa vya shule madaftari, pen za wino na penseli, wanatengeneza vifaa vya kuchezea kwa watoto kama vile midoli pamoja magari  ya kuchezea.


Jamaa pia hawajaawatupa masista duu - wamewatengenezea handbags, vitopu, nguo na viatu vikali vya kisasa maalum kwa wadada. Pia wamama wa nyumbani nao wametengenezewa vifaa vya kupikia kama vile majiko ya gesi, sufuria mpaka glass na vikombe tofauti vyote vikiwa na nembo ya FC Bayern Munich.


Kwa utafiti nilioufanya nimegundua klabu hii inategemea kwa kiasi kikubwa mapato yatokanayo na bidhaa wanazotengeneza kuweza kujiendesha hata kabla hawajayagusa mapato mengine yatokanayo na biashara nyingine wanazojihusisha nazo. Mamilioni ya EURO yanaingia kwenye accounts za klabu hii  kupitia biashara hii kwa sababu mamailioni ya washabiki wa Bayern Munich hapa Ujerumani na duniani kote wanaisapoti timu yao kwa kununua bidha mbalimbali zinatengenzwa na timu yao. Kwa mfano shabiki ambaye ni baba atamnunulia mwanae kuanzia vifaa vya shule mpaka midoli ya kuchezea yenye nembo ya Bayern katika kuhakikisha anaichangia timu yake kwa kununua bidhaa zao. Hii pia inaenda hivyo hivyo kwa watu wa rika na jinsia tofauti ambao ni wapenzi wa Bayern  mwisho wa siku timu yao inakuwa na uwezo mkubwa wa kifedha ambao unawapa mabavu ya kusajili mchezaji yoyote wanayemtaka kwa kuwa wanakuwa na fungu la maana la kununua na kuwalipa wachezaji. Hivyo kwa namna hiyo timu inapata maendeleo.

Hili ni somo kubwa kwa vilabu vyetu vikongwe Simba na Yanga, ambavyo kwa utaifiti mdogo nilioufanya ni moja kati ya vilabu vichache vyenye washabiki wengi barani Afrika, lakini vinaoongoza kwa umaskini na migogoro. Havina mipango endelevu na ndio maana kila siku vinazidi kuwa omba omba kwa matajiri ambao ni washabiki wa vilabu hivyo. 
Kwa mfano klabu ya Yanga ambayo kwa miaka kwa karibuni imekuwa katika mikono ya tajiri Yusuph MANJI / ebu jiulize kama wangekuwa wamemtumia Manji kuwatafutia mikopo ambayo wangeitumia kutengeneza vitu au bidhaa kama za Bayern Munich na kuviuza kwa mamilioni ya washabiki wao leo hii klabu hii ingekuwa tajiri kiasi gani? Hii pia hata kwa Simba inawezekana na kuweza kujipnga na kuwa na seriousness kwenye mipango yao. Naomba viongozi wa vilabu hivi waangalie mafanikio ya Bayern yaliyotokana na mipango thabiti na wachukue kama Challenge ili kuweza kutoka mfumo wa kimaskini walionao sasa na kuweza kwenda mbele kwa mfumo wa kisasa kama wenzetu huku nje. Endapo vilabu hivi vitaondokana na mfumo wa kizamani na kuiga vitu wanavyofanya wenzetu kwa hakika vilabu vitatengeneza fedha nyingi sana ambazo kama zikitumika vizuri zitaisadia kuziletea maendeleo vilabu hivi pamoja na kuendeleza soka la Tanzania kiujumla. 


Kutoka Munich Ujerumani Nwasilisha.

1 comment: