Search This Blog

Saturday, May 26, 2012

NAHODHA WA NIGERIA: KIFO CHA YEKINI KINA UTATA - UFANYIKE UCHUNGUZI - HAKUWA NA KICHAA.

Nahodha wa zamani wa Nigeria Segun Odegbami ameomba kufanyika kwa uchunguzi wa kina dhidi ya kifo cha RashidI Yekini.

Yekini aliripotiwa kutekwa muda mfupi kabla ya kifo chake, lakini chanzo halisi cha kifo chake bado hakijawa wazi.

"Walimchukua na kumteka kwa takribani wiki 3 na walipomrudisha, tayari alikuwa maiti - je kuna kitu gani kilitokea kipindi chote hicho walichokuwa kuwa nae?" -alisema Odegbami.

"Hakuna anayesema kwamba aliuwawa lakini chochote walichomfanya - katika jitahada za kumtibu kwa ugonjwa usio mkubwa ambao hakuwa nao - ndio kunaweza kuwa kumepelekea kuisha kwa uhai wake.

"Ndio maana tunasema uchunguzi inabidi ufanyike, ili atleast tujue nini kilisababisha kifo chake. Wapi alipokufa? Walimpeleka wapi? Nani alimtibu tena kwa ugonjwa gani?

"Huyu ni gwiji wa soka la Afrika - nyota na mtu ambaye amefanya watu wengi kupenda soka."

Polisi wa Nigeria wa Oyo State, mahali ambapo Yekini alikuwa akiishikabla ya kifo chake, wameliambia shirika la habari la Uingereza kwamba hakuna uchunguzi wowote uliofunguliwa juu ya kifo cha mchezaji huyo.

Odegbami ambaye pia alicheza na Yekini, anasema watu walikosea kuamini kwamba Yekini , ambaye aliishi kwa kujitenga katika miaka ya hivi karibuni, kwamba alikuwa akiandamwa na msongo wa mawazo.

"Watu wana mtazamo kwamba alikuwa ni chizi," alisema Odegbami, ambaye alikuwa na mawasiliano na Yekini mapema mwaka mwaka huu.

"Rahidi alikuwa sawa kiakili, alikuwa na afya, na fiti na hakuwa na tatizo lolote. Mtu wa namna hiyo hawezi kufa kiajabu ajabu na hakuna mtu anayejua amekufa vipi - wapi alifia na nini kilichomuua."

1 comment: